karibu

kwa habari moto moto

Sunday, November 1, 2015

Obama aiondoa Burundi kutoka kwenye AGOA

marekani imeiondoa Burundi kutoka kwenye mikataba yake ya kibiashara AGOA iliyowezesha mataifa ya Afrika kuingiza bidhaa zao katika soko la Marekani bila kulipa kodi.
Katika barua aliyoiandikia bunge la Congress , rais Barrack Obama ameelezea kuwa amechukua hatua hiyo baada ya kushuhudia kushuka kwa viwango vya demokrasia katika taifa hilo la Afrika ya Kati.


                                        pierre nkurunzinza
Burundi haijafanya jitihada zozote za kurejesha amani na utangamano'' Obama.
Obama alisema kuwa badala ya kuimarika kidemokrasia, Burundi inaendelea kushuhudia wapiganiaji wa haki za kidemokrasia wakikamatwa na kufungwa jela huku wengine wengi wakiuawa kwa kudai haki zao za kikatiba zifwatwe.
Aidha Obama ameelezea kuwa hatua ya serikali ya rais Nkurunziza ya kuwanyamazisha makundi ya wapinzani kwa kuwashika kuwaua na hata kuwatesa ni kinyume na maadili ya taifa linalodai kuzingatia demokrasia.
barrack obama wa marekani
credit to : bbc swahili
source:bbc wahili

No comments:

Post a Comment