karibu

kwa habari moto moto

Monday, November 30, 2015

Afrika bara lenye thamani kubwa duniani

Africa yetu na rangi nzuri tulie ipata kutoka kwa muumba wa mbingu na ardhi,, unaweza kushangaa kwanini nimelita bara la baraka ,kwa muono wa kawaida huwezi ona kitu ila ndio habari yenyewe ilivyo,afrika ni bara la pili  kwa ukubwa duniani na rangi yake ni weusi ambapo kuna rangi nyeupe inapatikana kaskazini mwa Afrika, haswa,libya,miri,moroco,tunisia na algeria hapo ndipo unaweza ona watu wenye rangi nyeupe kwanini nimezungunza kuwa ni bara lenye thamani kubwa duniani....na kwanini nisitaje kwa ulaya,au amerika?
afrika limetoa watu maarufu duniani karibuni 99% ya dunia ni watu weusi kwa wale ambao wanapenda kulaumu mungu kwanini haja tuopendelea na sisi watu weusi moja ya vitu alivyo tup ni hivyo watu wote maarufu huwa ni weusi na wanapesa zao kuliko weupe, mfano,,barack obama ,jay zee,beyonce,michel jackson,,,50 cent na wengine wengi  ambao sijawataja hao wote ni weusi,, tulicho nyimwa waafrika fikra pekee ambayo hicho ndicho kinacho tusumbua hadi wanakuja kutuchukulia mali zetu wanaondoka nazo bila kujua kisha baada ya kuondoka tuna gundua baadae kabisa na tunaanza kujilaumu,.
mungu amelipendelea bara hili la afrika kuwa moja ya maeneo yenye maliasili na vivutio vingi ambavyo vingetumika sawa sawa tuinge weza kuomba misaaada,, wafrika tunajiumiza kwa ubinafsi pindi mmoja anapopata nafasi hafanyi makosa kuiba na kujinufaisha wenyewe mfano mzuri Jamhuri ya muungano wa Tanzania tunaona tembo wanaibiwa wanawekwa katika ndege pia  vitu tunaviona ufisadi na habari nyingine za kuudhi hii yote inatokana na ubinafsi tulie nao wa afrika
tufanyeje ili tukomeshe vitu kama hivi viongozi waliopewa nafasi wafanye utaratibu wa kunufaisha  watu wote ili tutoke haopa tulipo na tuvuke zaidi libya ilikuwa miongoni  mwa  nchi zinazo nufaika na rasilimali zake kwakuwa hatuja zoea kupata raha wakaamua kumuua kiongozi wao alieta faida kubwa katika taifa lao



hii ni ramani ya bara la afrika tanznaia inaoneka afrika mashariki sehemu yenye maziwa 



Nikki wa pili atafuta director kutoka nje kuja kushoot video ya baba swalehe

Nikki w pili ametanabaisha kuwa atafanya video kubwa kwa mara ya kwanza katika hit song yake ya sasa baba swalehe ambapo katika nyimbo hiyo ame mzungunzia mwanaume asiye eleweka na anae kwepa majukumu kwa ajili ya mambo yasiyo yamsingi

 nikki wa pili wakati aki graduate degree yake miaka kadhaa iliyo pita

nikki wa pili ni mmoja wa wasanii wasomi zaidi nchini tanzania yuko tayari kumtAFUTA director mkubwa kutoka nje kwa ajili ya kutengeneza video yake .. wakati akifanya hayo kaka yake joh makini amepiga hatua kubwa katika video baada ya kutamba na video yake ya sasa dont bother aliyo mshirikisha aka ,,
nikki wa pili pia ametoa sababu ya kwanini video yake ya SAFARI  aliye washirikisha wakali kama ,jux,vmoney,joh makini,gako kuwa umbali wa wasanii hao ndio ulio fanya video hiyo kutotoka



dewji ashinda tunzo za forbes person of the year

Mkurugenzi mkuu wa METL mohamedi interprices Tanznaia limited , Mohamedi dewji ameshinda tunzo ya Forbes person of the year ,wakati wa upokeaji wa tunzo hiyo mohamedi ewji amesema tunzo hiyo ni masirahi ya wataznaia wote

siku chache zilizo pita orodha hiyo ya watu 500 matajiri zaidi barani afrika amabapo dewji alikamata nafasi ya 21 ktk orodha hiyo ilisomeka kuwa ana utajiri wa dola bilion 1.1

sheikhe ponda aonekana hana hatia

 Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa morogoro  imemuachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda aliyekuwa akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi na kesi ya jinai baada ya mahakama kutoridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka na hivyo kuonekana hana hatia

Makosa yaliyokuwa yakimkabili ni mawili ambayo ni kushawishi watu kutenda kosa, pamoja na kutoa matamshi yanayoumiza imani ya dini nyingine.

Hakimu wa kesi hiyo Mary Moyo amesema ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka haukujitosheleza hivyo mahakama hiyo imemwachia huru na rufaa iko wazi endapo upande wa mashitaka hautaridhika na hukumu hiyo.
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
                                     picha ya sheikhe ponda issa ponda

jaji alie kuwa anasimamia kesi hiyo  amemshauri sheikhe ponda kufungua kesi ya bakwatwa na kampuni agritanza limited aliyo uziwa eneo la waislam lililopo chang`ombe jiji dar es salaam na ame mshauri aisende kwa namna nyingine bali atumie njia ya mahakama,, pia imemuachia kwa kipindi cha miezi 12 kwa shart la kutofanya kosa lolote

source;mwanachi
source:east africa

Sunday, November 29, 2015

chicharito aweka rekodi

javier Hernandez ma jina maarufu chicharito tayari amevunja rkodi ya kuwa mchezaji kutoka mexico kushinda mechi saba mfululizo wakati rekodi zikivunjwa msimu huu kutoka ligi mbali mbali naye chicharito ameweka yake wakati rekodi hiyo alikuwa ina shikiliwa na hugo sanchez
                                   
chicharito ameondoka manchester united msimu huu nakutua buyern leverkusen akifanya vizuri tabgu atue hapo, wakati manchester united wakipata taabu mtu wa mwisho wa kufunga hiki kifaa kinafanya vizuri ujerumani na kuwa mchezaji wa kwanza kutoka taifa la amerika kufunga mechi saba mfululizo


Saturday, November 28, 2015

Jamie Vardy amevunja rekodi ya Ruud van Nistelrooy

Jamie Vardy ameweka rekodi ya kipekee katika ligi kuu ya england baada ya kufunga goli 11 katika mechi 11 alicho cheza msimu huu mfululizo rekodi hiyo ilishikiliwa na rud van nestoroy alie ichezea mamchester united
jamie vard
                 
jamie vard akishangilia goli katika mechi zilizo pita

vardy amekuwa na msimu mzuri tangu ligi ianze amezifunga timu zote 11 alizo kutana nazo msimu huu



dimond sina tofuati na bob junior na ngoma inafuata

Msani nyota wa bonge flava  Nasib Abdul  kwa jina maarufuku diamond platnumz amesema kuwa kwa sasa hana ugomvi na Bob junior na washa maliza tofauti yao kinachofuata kuna project kali inakuja kati ya bob junior na dimond platnumz


 star huyo wa nana akizungunguza na millard ayo ametanabaisha kuwa kwa sasa kinacho fuata ni kazi nzuri zaidi na mkataba wake na mashabiki ni kutoa kazi nzuri ambazo wanazifurahia pia amesema wazi amepatana na produced mwingine wa ngoma ya ukimwona mawazo maneck hivyo kuna nyimbo kali ya mapenzi inakuja mda si mrefu
milard ayo amemuuliza swali kuhusu colabo yake ya kimataifa kasema bado wanaseti vitu na amewaomba mashabiki wake kuwa na subira

Thursday, November 26, 2015

sauti sol watarajia kutoa video na alikiba

wakati wnanjiandaa kutoa album yao sauti sol wanatarajia kutoa ngoma yao mpya walio mshirikisha alikiba sauti sol
                                                 
                                   alikiba akiwa na sauti sol
vijana hao wakenya wamewashirikisha wasanii v-money ,joh makin katika nyimbo zao ambazo zitakuwa katika album ya pili baada ya kutoa hii.

katika ukurasa wao wa instagram wameweka picha hiyo

Tuesday, November 24, 2015

Tujue nafasi za viungo tusichangnaye

mara nyingi wachezaji wanao cheza nafasi ya beki huwa hawana matatizo ila mashabiki huwa wanachanganya kujua kuanzia namba sita hadi 11 hapo ndio huwa wanachanganya madesa,hapo wengi hawajui kuwa yupi kiungo mkabaji yupi anae google na yupi anae weza kukaba na kushambulia leo hii tutatoa mifano kwa wachezaji wa arsenal kwahiyo uta angalia jinsi wanavyo fanya na utalinganisha na timu nyingine utajua kuanzia leo

Defensive midfield hapa sasa tunawakuta viungo kama metheu flamin na fransic coquelin hapa mbwiga ana kwambia ngada tu ngada ndio hawa hapa akina poul schols patric viera hawa kazi yao kubwa kuzuiya mashambulizi na kupandisha timu inapo kuwa katika hatari kazi zao hawa jamaa kuzuiya tu ila haimanishi ndio hawafungi magoli ila kazi kubwa kuzuiya timu pinzani isipte katika sehemuya tatu ya timu yoa

                                                        fransic coquelin akiwa kazi
hawa viungo ni wachache sana siku hizi kiungo mkabaji wanafosi makocha kuwa weka kuwa defensive pia hapa tuna wakuta wakina morgan Schneiderlin au mikel obi wa chelsea na henderson wa liverpool
Holding midfield hapa wapo wengi sana kama kina arteta ,Aaron ramsey na wengine wengi hawa wana element kama za defensive kuwa tofautisha huwa inak uwa ngumu sana ila kama ukijua mpira utajua kamabisa japo pia defensive mara nyingine ndio hao holding

Attacking midfield  hawa wapo katika makundi mawili kundi lakwanza cental attack midfield (cam) yaani number 10 na left midfield (lam) yani namba 11 na right midfield (ram)  yaani 7 hawaa wote ni viungo kwa mfano kuna wakati ozil alikuwa anacheza 11 ila bado ana base sana katikati ya pembeni

hapa sasa una mkuta mtu kama ozil,chamberlen, alexis anchez,



                                                     alexix sanchez
Box box midfield hapa sasa  una mzungunzia mtu kama Aaron ramsey  na webgine wengi tu kama watu hao kama juan mata ,oscar

deep lying midfield huyu yupo karibu na kiungo mkabaji mfano wake santi cazorla yeye kuzuia kidogo na kupandiha timu


hapo utakuwa kidogo umepata kuona jinsi gfani hawa viungo wnavyo changanya ila huyu cazorla mara nyingine anakaa kama play make wa timu

                                         amini nyaungo


Monday, November 23, 2015

magufuli atoa tamko hakuna sherehe za uhuru december 9

Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania leo ametoa tamko kuwa sherehe za uhuru zifanyike kwa staili tofauti badala ya bajeti inayotumika siku hiyo itumike katika mipango ya kutengeneza maendeleoa mengine nchini
dk john pombe magufuli hapo wakati huo akiwa katika kampeni

raisi huyu mteule kupitia  chama cha mapinduzi ccm amesema  kupitia vyombo vya habari kuwa pesa na bajeti itakayo tumika katika sherehe hiyo zitatumika katika maendeleo mengine ya kitaifa hii ni katika kutekeleza ahadi zake mbali mbali alizo ziahidi ili kuboresha maisha bora na kauli mbiu yake ya hapa kazi tu
magufuli amepata kura milioni nane tofauti ya kura milioni mbili ya mshindikani wake edward lowasa kupitia chadema mwezi octoba mwaka 2015

Bbabu tale amesema dimond hatoongea kingereza katika nyimbo zake

Meneja wa dimond platnumz amesema hana mpango wa staa wa bongo flava naibu abdul kufanya ngoma kwa lugha ya kingereza watasubiri sana. akizungunza na kipindi cha xxl cha clouds fm kipengele cha 255 kinacho endeshwa na perfect crispin
Instagram media by babutale - Music makes money, however music also needs money. Big Tingz.
                                  babu tale akiwa na dimond platnumz 

amesema muziki wake umemtambulisha bila ya kuongea kingereza ukitizama ile ngoma ya my number one remix aliyo imba na davido haikuwa ya kingereza kwahiyo hakuna sababu ya yeye kuongeza

Friday, November 20, 2015

Rekodi za el clasico

Faraja na amani duniani kote kwa 55% wana huwa wana penda michezo haswa kandanda na kandanda kila mmoja ana kile akipendecho huyu anapenda chelsea kama makoleko kalibonge, huyu anapenda liverpool kama alikiba huyu anapenda barcelona kama dimond platnumz na yule arsenal kama ramadhani nongo na huyu manchester united kama saidi mpapuka sasham, hayo ni mapenzi tu na wengi sana wanapenda timu zao huku kila mmoja anakuwa na uwezo wa kuongea kama timu inapo fanya vizuri,
derby ziko nyingi sana kuna ac milan vs inter milan hii couple inapatikana italy, kuna buyern munich na borrusia dotmond hii ujerman, england ndio zipo nyingi sana kuna huku england huwa zile top four zikicheza huwa zina vuta hisia za watu na kama hujui vizuri derby za nchi hiyo utasema hizo ndio derby mfano man u akicheza na arsenal hii sio derby ila kutokana na ukubwa wa mechi hii utadhani derby wakti derby zao spurs kwa upande wa arsenal huku man city kwa upande wa man u na nyingine nyingi
leo hii tuna angalia derby ya hispania amabayo yafahamika kama  el clasico 

Rekodi zao sasa hadi sasa
katika el clasico timu zote zimefunga magoli 546 katika mechi walizo kutana tangu mwaka 1929 haddi sasa, kila timu imefunga magoli 99 ugenini. magoli mengi kufungwa katika mchezo mmoja ulikuwa mwaka 1935wkati real madrid ilipo ifunga barcelona  magoli 8-2 na mwaka 1943 timu hizo zilipo toka sare ya goli 5-5 magoli ya mapema katika derby hiyo  karim benzema alifunga sekunde ya 23 decembe 2011
toka mwaka 1929 barcelona imeshinda mara 67 wakti real madrid imeshinda mara 71
katika mchezo wa leo leonel messi atakosekana kwa kuumia  kiazi cha mguu wakati wachezaji ghali watano wakichzea wote wataweka historia neymar,suarez,ronaldo .james na bale wana kamailisha kiasi cha  $367m


Tuesday, November 17, 2015

walifanya haraka

Leo katika ukurasa hu wa chambertalkshow1,blogspot inakuletea uchambuzi yakinifu wa wachezaji ambao walmefanya haraka kuondoka katika timu ya arsenal orodha ipo kubwa ila leo tuta wachambua watatu kati ya hao
1.Alexander Hleb amezaliwa 01 may 1981  nchini Soviet union ana urefu wa futi 6 na nch 1 amecheza timu nyingi sana ila arsenal ametua msimu wa 2005-2008 amecheza kwa mafanikio makubwa sana akiwacheza kama winger ya kusoto au kulia kuyokana na mpangilio wa mwalimu arsenal  amecheza mechi 89 na kashinda magoli 7


                                   

                                                    alexander Hleb akiwa arsenal
hakuna asiye jua kwa walie mtizama wakati anacheza timu ya arsenal kipindi hiko amecheza vizuri sana na alikuwa na kasi na msaada mkubwa sana hleb amefanya haraka kuondoka sababu kipindi hiko ndio alikuwa katika moto na kiwango cha juu akawahi kutondoka na kutimkia barcelona mwaka 2008-2012 lakini barcelona hakucheza sana alikuwa anatolewa kwa mkopo hadi anaondoka timu hyo
Maisha ya Hleb sasa ya mpia yako katika timu ya bate bolisov

2.Metheu Flamin mzaliwa wa ufaransa 7 march 1984 ametua arsenal mwaka 2004-2008 flamini alikuwa namba sita hodari sana alikuwa anapiga mashuti anahamasisha mbele za wachezaji wenzake japo hakuwa kapten wa timu mchamngo wake ulikuwa mkubwa sana ndani ya emirate kipindi hiko ,, flamini kilicho mtoa arsenal tamaa ya kuongezewa mshahara

   
                                                                      metheu flamin
ameondoka wakati mashabiki wa arsenal wanamuhitaji hakuna aakae kataa kwa kipindi hiko flamini ana kumbukwa kwa vituko vyake vya kukata jezi ikiwa ya mikono mirefu  ama kwa hakika hili llikuwa jembe sana ila amewahi sana kuhama timu hiyo yenye makao yake makuu mji wa london england, ameondoka arsenal mwaka 2008-2013 kaenda Ac milan nako hakuonesha tena zile cheche zake  japo arsenal amecheza mechi 102 na kafunga goli 7 wakti milani kacheza mechi 97 kafunga goli 7 pia mwisho wa msimu wa 2013v wamemuachia huru na kukubali tena kula matapishi yake kwa maana ya ule mshahara alie ukataa umeshushwa zaidi

3.alex song huyu nae kiungo hodari sana kipindi hiko amezaliwa 7 september 1987 nchini cameroon katua arsenal 2005-2006 kwa mkopo baadae wamemchukua moja kwa moja mwaka 2006 amecheza michezo 138 na amefunga magoli  7  huyu pia alikuwa na taama za kucheza na lionel mesi timu moja maana upendo wake kwa mchezaji huyo ulidhihirika hata kabla haja hama timu hyo


                                                       alex song 

naye amehama arsenal wakati bado anahitajika hivyo kuweka orodha ya wachezaji wengi wa arsenal walio hama wakati wanaweza na wangine


Job ndugai ndiye spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania

job ndugai ndiye spika wa bunge la 10 la jamhuri ya muungano wa tanznaia mara baada ya kuibuka mshindi wa kiti hicho kwa 70% ya kura zilizopigwa mchana wa leo, wagombea walikuwa wengi ,moja ya mgombea wa kiti hiko alikuwa hashim rungwe ambae yeye hakutokea bungeni katika kujieleza

mheshimiwa spika  job ndugai moja ya picha zake

ndugai ni mbunge teule wa jimbo la kongwa dodoma ,katika bunge lililopita alikuwa naibu spika wa bnge akiwa chini ya mama anna makinda  ambae aliweka historia ya spika wa kwanza mwanamke Tanzania tangu ipate uhuru

Monday, November 16, 2015

lambert kocha mpya aston vila

Kocha wa zamani wa atoni vila paul lambat ame amechukuwa kibarua kipya kaitka timu yasoka ya blackburn   baada ya gary bowyer kufutwa kazi mwezi february mwaka huu na aston vila


 lambert amefukuzwa kazi astoni vila mara baada ya kucheza mechi 10 na kusinda mbili kazti ya hizo

Sunday, November 15, 2015

dimond paltnumz na vanesa mdee wameshinda tuzo za afrima

Mwanamuziki Dimond platnumz na vanesa mdee wameshinda tuzo za afrima award zilio fanyika nchini nigeria usiku wa jumapili tarehe 15.11.2015 dimond platnumz ameshinda tunzo tatu ambazo ni artiste of the year,best male artiste in east africa na wimbo bora wa afrika
diamond afrima

dimond kipengele cha afrika mashariki alikuwa ana gombania tunzo hiyo sambamba na alikiba,jose chamilion,jaguar na wengine ,wakati msanii bora wa mwaka alishindana na davido,alikiba,jose chamilion,wizkid, huku wimbo bora wa mwaka akiwa na alikiba,davido,wizkid,sarkide na wengine
wakati huo huo v-money vanesa mdee yeye amechukua wimbo bora wa afro pop hawajui
vee

akiwa akishindana na yemi alade na wasanii wengine wakubwa, hivyo kufanya tunzo nne zimefika afrika mashariki


magufuli afuta kitengo cha lishe ya raisi ikulu

Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dkt Joh Pombe Magufuli ameendeleza ahadi zake ya kupunguza vitengo visvyo na faida katika uongozi wake hii ameisema wakati wa kampeni zake moja ya ahadi zake ilikuwa kupunguza baraza la mawaziri pamoja na vitengo  vingine ambavyo havina maana na faida kwa nchi,


moja ya vitengo alivyo viondoa ni kitengo cha chakula kwa rais ikulu pamoja na kitengo cha  kukaribisha wageni binafsi ameviondoa vitengo hivyo na  sasa walio kuwepo amewarudisha katika vitengo vya awali, hu ni muendelezo wa ahadi zake alizo ahadi

source dar24


Friday, November 13, 2015

sichukui form ya spika maneno ya anna makinda

spika wa bunge lililopita mheshimiwa Anna makinda ametanabaisha kuwa hatochukua form ya kutaka uspika ,mh Makinda amesema huu ni wkati muafaka wa yeye kustaafu mara baada ya kulitumikia bunge na serikali zaidi ya miaka arobaini ya uongozi hivyo amewaacha wale walio kuwa wana tia mashaka ya yeye kugombania tena spika wa bunge


ANNA MAKINDA AKIWA BUNGENI
makinda ni mwanamke wa kwanza Tanzania kushika wadhifa wa uspika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanznaia tangu taifa hilo lipate uhuru 1961, amesema kuwa huu ni wakati rasmi wa kustaafu ikiwa raisi alie maliza muda wake mwaka huu dkt jakaya kikwete ni rika lake ktk uongozi kama kikwete amestaafu na yeye hana budi kuwaachia wengine labda kuna kitu watafanya kwa ajiri ya taifa letu


qchilla na tid kama zamani

aboubakari katwila almaaruf q-chila na Khalid mohamedi TID wameamua kuondoa ugomvi wao uliopo na kuamua kurudi kama zamani, wakizungunza na kipindi cha clouds fm wakati q-chillah akitambulisha ngoma yake mpya alo mshirikisha tid


qchila akiwa na  tid moja ya ngoma zao zamani nilikataa

qchila amesisitiza wakongwe wasaidiwe washikwe mkono kwani wameisaidia bongo flava kufika hapa aidha qchila ametanabaisha kuwa baada ya kutoa video ya ngoma hiyo ndipo project yao ya pamoja itarejea

Tuesday, November 10, 2015

wayne rooney katika miieleka

baada ya kukosa kurudi katika  ubora wake nohodha wa timu ya taifa ya england na manchester united wayne rooney ameonekana katika mieleka akishuhudiamichuano hiyo ya WWE RAW huku wayne rooney akimpiga kibao wade barret  na shamus kushinda pambano hilo

Wayne Rooney lands a theatrical slap on Wade Barrett after being called out by the wrestler at WWE RAW in Manchester


wayne rooney akimchapa kibao barrete

Excitement: Wayne Rooney was part of WWE's RAW live show from Manchester. His son Kai can be seen bottom right
                                               wayne rooney 

katika pambano hilo shemus kashinda kwa technical baada ya barret kuchapwa kibao na shemus kutumia vizuri nafasi hiyo kumbana na kushinda


wayne rooney akimchapa kibao barrate





christiani bella amfuata mzee wa ekotite coffi olomide

wakati tuna subiria collabo nyingi na tukiwa bize kwa wanamuziki wetu baada ya lumaliza kutengeneza video yao ya nagharamia  christian bella akiwa na ali kiba sasa bella ameenda jamhuri ya congo kufanya collabo nyingine na mkali wa ekotite koffi olomide


christian bella akiwa na koffi olomide

ktika page zao za instagram aeweka picha hizo  wakiwa studio mkali huyo wa amerudi

wenger na jamie vard waibuka na zawadi za mwezi england

arsene wenger amechaguliwa kuwa kocha wa mwezi 10 baada ya kufanya vizuri mwezi huo,, akaifunga manchester united ,3-0,everton 2-1 na mwisho swansea city 3-0 hivyo kufanya kuto fungwa mwezi huo


arsene wenger akibeba zawadi yake
wakati huo huo katika kutoa zawadi hizo mchezaji bora wa mwezi huo ni jamei vard
Leicester's Jamie Vardy has been named the Barclays Premier League Player of the Month for October

vard akishikilia zawadi yake

jaie vard amevunja rekodi mbli mbali msimu huu mara baada yakufunga mechi 11 mfululiza na kufanya kuwa mchezaji bora wa mwezi huo vard amefunga goli nne

joh makin ft aka wa south africa

katika kuhakikisha muziki wetu unaenda mbali haswa baada ya muziki w kufoka foka kuonekana kuzorota japo ndio haswa wenye ujumbe katika maisha halisia rappa kutoka kaskazini JOH MAKINI ata itoa leo ngoma yake mpya aliyo mshirikisha rappa mwingine mkali AKA wa afrika kusini
Joh na AKA MTV

intagram page ya joh na mtv base wameweka picha hiyo juu na chini wameandika speaking new  today at 16:00wat,17:00, 18:00 JOH MAKI FT AKA ,, kila laheri joh

Monday, November 9, 2015

moyes afutwa kazi real sociedad

kocha alie jizolea sifa nyingi england katika timu ya  everton david moyes , yamekuta tena yaliyo mkuta manchester united moyes 52 amefututwa kazi baada ya mwenendo mbovu wa timu hiyo ambayo msimu ulio pita aliishia nafasi ya 12 na bod ya timu hiyo kuamua kusitisha mkataba wake


                                  david noyes akiwa mazoezin
nafasi yake ataikaimu kocha msaidizi  billy mckinlay,moyes alichukuliwa na timu hiyo msimu ulio pita 2014 baada ya kutimuliwa kazi manchester united

dimond platnumz awaweka tayari mashabiki wake

dimond platnumz amewaasa mashabiki wake kuwa nyimbo atakazo toa mwaka huu itakuwa historia kubwa na zitakumbukwa hadi mwisho wa uhai wake,


                   dimond platinumz  akiwa moja ya picha zake


hii ndio pot yake katika tweeter Chibu Dangote  @diamondplatnumz
Nyimbo na Videos nnazoenda kuachia mwaka huu, zitakuwa ni Historia na Kubaki kumbukumbu hadi siku ntapozikwa....
staa huyo wa hit songs kali ya NANA ameandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa tweeter

vijana chini ya miaka 17 wa nigeria watetea ubingwa wao wa dunia

nigeria imeteta ubingwa wake wa dunia mara bada ya kuifunga mali ushindi wa bao 2-0 nigeria wametetea ubingwa wao mara baada ya mwaka jana kunyakua ubingwa huo wa dunia chini ya miaka 17


wachezaji wa nigeria chini ya umri wa miaka 17 wakiserebuka ushindi wao

Sunday, November 8, 2015

mesut ozil aweka rekodi bpl

kiungo mshambuliaji wa arsenal ameweka rekodi baada ya kutoa usaidizi(assist) 6 mfululizo na kutoa pasi za magoli michezo 11 ambapo hakuna yeyote alie wahi kufanya rekodi ,ozili alie sajiliwa kwa dau kubwa katika histotia ya timu ya arsenal kwa dau la paundi 42 mwaka 2013


ozil amevuka kiwango cha kutoa nafasi za magoli alizo funga za msimu ulio pita ambapo alitoa assist 9 ,,hadi sasa ozili amefikisha 10 bado 10 nyingine afikishe rekodi ya thierry henry,

wakati huo huo arsenal imetoa sare katika uwanja wake wa nyumbani dhidi ya spurs ambayo ilianza kupata goli kupitia harry kane goli la kusawazisha la arsenal lilipatikana kupitia gibbs aliengia kuchukua nafasi ya joel campbel hivyo kufikisha alama 26 sawa na manchester city alie mzidi kwa magoli

muziki wetu

diamond platnumz ni kijana wa kitanzania jina lake kamili ni nasibu abdul amezaliwa 02/10/1989 dar es salaam tandale kwa mtogole , hii hakuna isye ijua, kwanini nimeamua kuandika makala fupi inayo muhusu superstaa wetu huyu wa bongo flava


siku zote jitihada ndizo zina muweka mtu mahali popote pazuri bila shaka dimond amefanya jitihada nyingi za kujikwamua mwenyewe na kuonesha mfano kwa wengine wanao mzunguka,, dimond ni kijana ambae ametoka katika familia ya kawaida na kuwa famili kubwa kwa maana yenye mafanikio,,
kwanini diomond katika makala hii,,nasibu abduli a.k.a mond bin laden kama anavyo jiita huwa haachi kutumia fursa pindi aipatapo ametoka na nyimbo ya nenda kamwabie ambayo ameirekodi kwa bob junior baada ya hapo katoa hit song nying sana,, nalia na mengi,, nitarejea,,mawazo nataka kulewa.kesho na nyingine nyingi



amepata fursa moja na akaitumia vizuri hivi sasa diamond dunia nzima anafahamika na sichelei kusem kuwa yeye ndiye alie shika bendera kuiperusha katika tasnia ya muziki wa bongo flava kujulikana zaidi ulimwenguni kote ,,kwa kipindi cha miaka miwili ambyo ndio kajulikana kimataifa zaidi baada ya kutoa rimix ya #mynumberone akimhiriksha davido

sasa hivi ana tunzo zaidi ya 50 katika kabati lake hizi za nyumbani na nje ya nje hiv wiki kadhaa zilizo pita amemshinda miss india na kuchukua yye zawadi ya mtv ema ambayo nikubwa akiwabwaga  wasanii wakubwa wengine wakina davido,, wizkid katika kinyang`anyiro cha awali kabla ya kushindana na miss india

nini nataka kusema magufuli kaja na slogani ya hapa kazi tu,, ila hii slogani watu wasiitafiri vingine lazima atundee kazi kutokana na slogani yake lakini jitihada kubwa zipo kwako wewe mwenyewe kijana kuhangaika huku na kule kuweza kupata ajira kisha uwezeshwe

dimond kanionesha mfano mkubwa sana wa jitihada zake na kutuonesha vijana wengi kuwa tunapo pata fursaa hatuna budi kuzi shikilia na kuzifanyia kazi
hivi sasa dimond ni milionea ule msemo wa kingereza unao sema FROM ZERO TO HERO ndio haswa dimond alicho kifanya

bila shaka dimond jitihada zake za kimuziki zinaonekana na uongozi wake pia tunaona wanacho kifanya na  hivyo kufanya wengine waweze kuchakarika ili mambo yaende kama mfupa ushalika sasa wasanii mbali mbali mbali wanatka kufanya collabo na wasanii wa wa kitanzania ku juhudi binafsi za kijana wetu

kwanini kuna team,, team nzuri endapo zinge tumiwa vizuri namini katika watanzania milioni 45 nusu yake wanatumia mitandao ya kijamii kama siya pili kwa afrika katika utumiaji huo basi ya kwanza kulingana na idadi hiyo,,

team nzuri ila hizi timu tusizitumie vibaya kwa maana ya ilivyo sasa maana mimi nawewe unaye soma unae unaemshabikia katika hawa wanao shindanishwa kwanini tutukanane wakati tayari


muziki wetu ushaenda mbali kupitia huyu mtu na wengione wengi,,

uzuri wa hizi team ni pale tunapo ona kila mmoja anajitahidi sasa kutafuta uwezekano ili atusue zaidi lakini tusapoti wote,, na watanzania tumelemaa kwa alikiba na dimond pekeeake wakati kuna wasanii wengine kama belle9 ..ben poul na wengine kwanini tusiwapush wote ili mambo yaende na muziki wetu ukue zaidi

Saturday, November 7, 2015

pires ametaja kikosi chake bora sanchez,koscielny,cocquelin na cazorla waingia

hii ni first eleven ya mchezaji mkongwe wa arsenal aliye itoa kama  team yake ya wakati wote,, kama wachezaji wanao cheza sasa hivi wange kuwepo ni wachezaji wanne wa kikosi cha kwanza ndio wanfeweza kuanza katika kikosi chake
mara nyingi wachezaji wakitaja vikosi vyao bora kwa wapendao sasa pires ametaja kikosi bora

kocha :robert pires


Magufuli awaita makatibu wakuu kuboresha utendaji wa kazi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa Ikulu ya Dar es Salaam amefanya kikao na Makatibu wakuu, Manaibu Makatibu wakuu, Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kutoa uelekeo wa Serikali anayoitaka mara baada ya kuapishwa.

“Nataka Serikali iendelee kwa nguvu zote na katika kutekeleza dhana ya ‘HAPA KAZI TU’ na viongozi kuzingatia na kukumbuka ahadi nilizotoa ili zianze kuonekana na kufanyiwa kazi mara moja” Rais Magufuli amesema.


Katika Kikao chake, Rais ametoa mwongozo na kusisitizia kuwa ni lazima kila mtendaji Serikalini kuuzingatia, kufuata sheria na taratibu ili taifa lisonge mbele kwa ufanisi zaidi.
Katika kikao hicho Rais ameelekeza mambo kadhaa ambayo watendaji hao wanapaswa kuyasimamia, kuyawekea mikakati na kuyapanga vizuri ili atakapo teua Baraza lake la Mawaziri mambo hayo yawe tayari ili Mawaziri watakaoteuliwa waweze kuyasimamia bila kukosa.


Mambo hayo muhimu ni kama ifuatavyo:
Kuanzia mwezi Januari mwaka 2016, wanafunzi wote wanaoanza shule watasoma bure bila kulipa ada, Katika jambo hili, Rais amewataka watendaji kuanza kuliwekea mikakati tayari kwa utekelezaji
Suala la mikopo ya wanafunzi nalo lifanyiwe kazi na mipango yake ikamilike kwa ajili ya utekelezaji mzuri zaidi

Amefuta safari zote za nje ya nchi kuanzia leo hadi hapo atakapolitolea suala hilo maamuzi mengine na kueleza kuwa shughuli zote zinazotakiwa kufanywa nje ya nchi zifanywe na kusimamiwa na mabalozi wa Tanzania wanaowakilisha nchi huko nje.

Pengine patokee jambo la dharura sana na hata hilo lazima kibali kitolewe na Rais au Katibu Mkuu Kiongozi. Badala yake Rais amewataka watendaji hao kufanya zaidi ziara za kwenda vijijini ili kuzijua na kutatua kero za wananchi wa Tanzania.

Katika Kikao hicho, Rais amemtaka Kamishna wa TRA, Ndugu Rished Bade kusimamia kwa makini zoezi la ukusanyaji wa mapato nchini na kuhakikisha kero ndogo ndogo kwa wananchi lianze kutekelezwa kama alivyo ahidi kwa kufanyiwa kazi mapema zaidi.

Rais ameitaka TRA kukusanya mapato hayo kutoka kwa wafanya biashara wakubwa zaidi na wale wanaokwepa kodi bila kuogopa mtu wala taasisi yoyote hapa Tanzania na kusisitiza kuwa katika Serikali hii wa kutoa maamuzi vinginevyo zaidi ya haya ni yeye Rais ama Makamu wake.
Rais Magufuli pia ameagiza usimamizi katika suala la manunuzi ambalo limekuwa likitumika vibaya na kuwa mwanya wa kuibia Serikali kwa watu kuongeza bei ya vitu hata kama ni vya bei ndogo kabisa katika jamii.

“Ikitokea suala hilo likagundulika kwa watu kuongeza bei ya vitu, watendaji watawajibishwa mara moja”. Rais amesema, na kuwataka watendaji hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo na kuzingatia maadili mema ya kazi.
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
7 Novemba, 2015

alikiba kufanya video mpya marekani

alikiba ametua marekani kushoot video mpya baada ya kupata mawasiliano na video quuen kutoka marekani,, hii leo ameonekana akipiga picha akiwa na video queen huyo wa chriss brown ,,nikki minaji, rihana,,, katika page yake ya instagram  yaani
@officialalikiba ameweka picha hizo
12224581_1515849052072580_297854157_n



alikiba akiwa na video quuen huyo aliya janel

11917768_909457925806074_2034597923_n
picha hizo alikiba akiwa na video  quen huyo


11262715_974913289232700_897703213_n
alikiba hapo akifanya yake
source : alikiba instagram

Friday, November 6, 2015

magufuli afanya ziara ya kushtukiza wizara ya fedha 6 hawakuwepo kazini

Rais mteule wa jamhuri ya muungano wa tanzania amefanya ziara ya kustukiza katika ofisi za fedha na kukuta wafanyakazi 7 hawapo kazini hivyo amewataka wajieleze kila mmoja ambae hakuwepo walikuwa wapi?




huo ndio msafara alio ufanya ghafla, katika mitandao ya kijamii wanaonesha kupata imani taratibu ya mhe mafuli wengi wao wana mpongeza kwa tukio hilo ,, lakini pia itawafanya wafanya kazi kukaa kazini na kufanya kazi


huo ndio msafara wake leo hii dk mafufuli yuko katikati

samweli sitta na zungu mchuano mkali

katika majina ambayo yatatatzamiwa yatakuwa naupizani mkubwa kuwania kiti cha uspika wa bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania ni samweli sitta na mhe zungu ambao kwa pamoja ndio majina yanayo tajwa kuchuana vikali katika kinyang`anyiro hiko

Samuel Sitta.png




umahiri wa samweli sitta unafahamika katika bunge la tisa ambapo aliweka usawa na  umoja katka bunge hilo bunge lililopita alikatwa kwa kigezo  cha kumpisha mwanamke naye auongoze , akizungunza katika kipindi cha azam tv sitta amesema hato kubali kukatwa tena  kinacho takiwa anae pita ndiye atakaae ongoza



zungu yeye alifanya vizuri bunge lilo pita  kwa kuachiwa kuwa mwneye kiti ali tenda haki  ahata wapinzani walipenda  uongozi wake
 hivyo kutakuwa na umuhimu mkubwa katika kinyang`anyiro hiko




masanja wa ze commedy ajitosa kuwania ubunge ludewa

masanja mkandamizaji wa kikundi cha ze comedy amejitosa rasmi kugombea ubunge jimbo la ludewa  baada ya alilokuwa deo filikunjombe,

Masanja Kwenye Foleni ya Ubunge Ludewa.. Ataacha Komedi? Asipopita? Viatu vya Marehemu?
masanja mkandamizaji

wagombea wengi ni,deo ngalawa, evearisto mtitu,zefania jwahula,james mgaya, johnson mgimba na simon ngatunga

arsenal hoi kwa buyern munich yapigwa 5-1

arsenal yaangukia  pua mara baada ya kuapishwa goli 5-0 na buyern munich mchezo ambao ulikuwa wa upande mmoja, arsenal imeingia katika mchezo huo bila ya nyota wake watatu wa kikosi cha kwanza, hector bellerin,theo walcot, aaron ramsey



nacho monreal akiwa katika harakati za mashambulizi
lewandowsk ndiye alie anza kufungua karamu ya magoli mara baada ya kufunga kwa kichwa huku mabeki wa arsenal wakiongozwa na per metersacker kudhania ameotea



lewandosk na debuchy
 goli la pili lilipatikana kupitia alaba baada yakupiga shuti kali lililo mshinda goli keeper wa arsenal petr chech ambaye ndiye alikuwa nyota wa mchezo,, magoli mengine yamepatikana kwa arjen ruben mpira wa kwanza tangu aingie ,thomasi mullar alie gunga mawili

goli la arsenal limepatikana kupitia olivier giroud