karibu

kwa habari moto moto

Monday, October 12, 2015

WANATUCHORA

MAKALA

Ifikapo tarehe 25/10/2015 tukio zito la kihistoria Tanznaia,, ambapo kila mwananchi ataamua nani ampe kura ili ashike hatamu ya kuiongoza nchi yetu ya tanzania kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, naamini mwaka huu hakuto kuwa na makosa katika kumchagua mtu sahihi wa kuweza kupewa dhamana ya watu milioni 45 ya watanzania, ni chaguzi ya awamu ya tano kupitia vyama vingi,,akipatikana raisi atakuwa raisi wa awamu ya tano pia

Huu ni uchaguzi ambao una changamoto na hisia kubwa sana ukilinganisha na chaguzi zote zilizo pita kuanzia mwaka 1995 baada ya uchaguzi mkuu wa kwanza kuanza kupewa nafasi kupitia vyama vyingi. nikikurudisha nyuma mwaka huo vilikuwa vyama vingi sana,, lakini vyama vilivyo kuwa na mvuto wakati huo vilikuwa .. NCCR mageuzi,CUF  hivi vilikuwa vina chuana vikali na chama tawala cha mapinduzi (ccm)

mshindi akawa benajamini mkapa kupitia chama cha mapinduzi (ccm) vyama vingine vilizidi kushamiri na kuweka mizizi taratibu, na kuteka hisa za wanacnhi wengi . naweza kudiriki kusema chama cha demokrasia na maendeleo chadema,, nacho kilitokeza vizuri  kuanzia mwaka 2000 imeweza kuchukua hisia nyingi na 2005 walipo msimamisha mwenyekiti wao mh freeman mbowe

kiliweza kutikia na kuweka misingi imara  ilishika namba mbili katika uchaguzi huo wa raisi ,, kuanzania hapo ikawa ndio chama pinzani sasa chenye mashabiki na wameweka imani yao kuwa kitaweza kuwaokoa  katika swala zima la uongozi

kwanini nasema wana tuchora, Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo tuna amani ya kinadhalia kwa maana amani ya vita hatuna japo amani ya maisha kwa maana ya kazi nzuri na maisha ya milo mitatu haupo, ila hata hiyo amani tuliyo nayo  pia nimuhimu sana katika taifa letu tulivu

nchi nyingi barani africa wana TUCHORA na kutaka watuweke katika historia ya nchi yenye machafuko duniani, wana subiri je na sisi tutaingia katika machafuko?  wengine washa ongea mapema mfano raisi wa Rwanda alisema mapema, wakti lowasa anahama ccm kuhamia chadema kuwa tutaona  Tanznaia ya mwaka huu.

hivyo hivyo nchi nyingi zilizo tuzunguka nazo zina tuangalia na  nina amini wanaomba dua usiku na mchana ili waone nasie tunaingia katika machafuko ya wenyewe kwa wenyewe kama walivyo wao,, hii inatoka kana na siasa ya mwaka huu kuwa na mvuto wa aina yake haswa baada ya kuhama hama wana siasa kutoka huku kwenda huku,,

mwisho wa siku wana tuchora, majibu yao ni rahisi mno wajue kuwa Tanzania ni ile ile ya miaka yote mungu ndiye anae ongoa taifa hili na waache watuchore ila wamefeli,, uchaguzi huu utatakuwa wa haki na usawa haswa baada ya nec chombo kinacho simamia uchaguzi kusimama imara na kuwatoa hofu kuhusu uchaguzi huu.. na naamini yoyote atakaye shindwa ata kubali tena kiroho safi

na hii itaitwa tunawakomeshe wanao tuchora kwa jicho la ubaya ..

imani yangu kubwa yoyote atakaye chaguliwa kuwa kiongozi wa nchi awe chadema, awe wa ccm, awe wa act au chauma na udpp atatekeleza yale yote ambayo tume yaagazia,,, nina imani kubwa japo fainali naiona kati ya MAGUFULI na LOWASA,, yoyote katika huyu

mungu ibariki TANZANIA,, Mungu wabariki wananchi wake,, mungu ibariki siku ya tarehe 25/10/2015 Aamin ,

wasiliana namini kwa kukosao ..maoni au maelezo mengine kupitia 0763315006/0717519981 au aminiamali@yahoo.com

No comments:

Post a Comment