Cristiano Ronaldo sasa ndiye mfugaji bora wa muda wote wa Real Madrid akifunga bao moja Madrid ikiichapa Levante mabao 3-0 kwenye La Liga. Ronaldo, 30, alifunga bao lake la 324 kwenye La Liga katika mechi 310 akiwa na klabu ya Real akimpiku Raul. Ronaldo alitangazwa rasmi kuvunja rekodi hiyo bada ya kufunga kwa shuti kali nje ya box huku mabao mengine ya Madrid yakifungwa na Marcelo na Jese. Mshambuliaji wa New York Cosmos Raul, ambaye atastaafu soka baadaye mwezi Novemba, alikuwa mfungaji wa muda wote wa Real ambapo ilimchukua mechi 741 kufunga mabao 323. Fowadi wa Wales Gareth Bale alipumzishwa wakati wa mapumziko dhidi ya Levante nafasi yake ikitwaliwa na Lucas Vazquez Real ikipanda kileleni. Barcelona inakamata nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao baada ya kuichakaza Rayo Vallecano

picha juu ronaldo akiwa ana chukua tunzo
No comments:
Post a Comment