Timu ya soka ya real madrid ya uhispania imeanza fujo katika timu ya soka ya arsenal ya jijini london mara baada ya kuwa tumia salamu za kuhitaji huduma za nyota wao raia wa chile alexix sanchez hii inatokana na faida ya kujituma na kuupenda mchezo wa soka wa mchezaji huyu mwenye miaka 27
sanchez ambaye alisaini mkataba wa miaka miwili arsenal msimu ulio pita wa 2014-2015 aliiwezesha timu hiyo kushika nafasi ya tatu ligi kuu ya uingereza huku akifunga mabao 25 ya mashindano yote msimu wa kwanza wa usajali wake klabuni hapo , pia sanchez aliweka kimiani magoli 15 ya ligi kuu ya nchi hiyo
sanchez alisajiliwa na arsenal akitokea barcelona kabla ya hapo alicheza udines ya italia, ni mchezaji wa kwanza kufunga hat trick nchi tatu tofauti, yaani italia,hispania, na uingereza.
sanchez alianza kusua sua mwanzoni mwa msimu huu alianza kufungua akauti ya magoli pale alipo anza kufunga magoli matatu na Leicester city baadae kuifunga manchester united bao mbili katika ushindi wa goli tatu, kisha kushine na kuifungia timu yake ya taifa goli mbili,, sanchez hivi sasa anafanya vizuri sambamba na walcot katika timu ya arsenal
hata hivyo sanchez leo katika link ya arsenal sanchez alimesema anayafurahia maisha ya emirate na hato kuwa na amani kuhama timu hiyo kwa kipindi hiki
real madrid sio mara ya kwanza kutaka huduma za wachezaji wa arsenal msimu uliopita wali mtaka laurent koscielny
arsenala wanatarajia kumuongea mkataba mpya mchezaji huyo na kuwa mchezaji anaye lipwa zaidi emirate, arsenal itakutakana na watford ligi kuu ya uingereza jumamosi hii kabla ya kukutana na buyern munich katika klabu bingwa ulaya,ambapo hadi sasa klabu hiyo haina alama yoyote baada ya kupoteza michezo miwili ya awali na wachambuzi wa micheza kuhoji muelekeo wa arsenal uefa mwaka huu
No comments:
Post a Comment