karibu

kwa habari moto moto

Sunday, October 18, 2015

EPL: Watford 0-3 Arsenal: Ozil balaa Arsenal ilicheza vizuri hasa kipindi cha pili na kufanikiwa kuiibuka na ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Watford na kukamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa Premier League. Alexis Sanchez 

sanchez

alifungua karamu ya mabao baada ya mapumziko baada ya Mesut Ozil kufanyiwa madhambi.  Olivier Giroud akafunga bao la pili, kabla ya Aaron Ramsey kufunga bao la tatu huku likiwa bao lake la kwanza msimu huu. Watford walikosa nafasi ya kupata bao kipindi cha kwanza baada ya Odion Ighalo kupiga shuti lililokosa uelekeo.  NYOTA WA MCHEZO - MESUT OZIL (ARSENAL) Mesut Ozil alipiga pasi sita muhimu (ikiwemo pasi mbili zilizozaa mabao) - zaidi ya 

Mesut ozil

mchezaji yeyote wa Arsenal DONDOO UNAZOTAKIWA KUZIFAHAMU Watford haijashinda mchezo wa Premier League mwezi Oktoba (D4 L6). The Gunners imeshinda mechi sita za karibuni dhidi ya Hornets kwenye mashindano yote, ikijumuishwa na michezo mitano ya mwisho kwenye Premier League. Watford imefungwa mabao mengi kwenye mchezo huu (matatu) sawa na mabao waliyofunga kwenye mechi sita ilizocheza uwanja wa Vicarage Road. Ramsey 

aaron ramsey

alifunga bao lake la kwanza msimu huu kwenye Premier League, baada ya kushindwa kufunga katika mashuti 26 (yakiwemo yaliyozuiliwa) msimu wa 2015-16. Mshambuliaji wa Watford Troy Deeney anaongoza kwa kupiga mashuti mengi bila kufunga kwenye Premier League msimu huu (mashuti 23 yakiwemo yaliyozuiliwa). KINACHOENDELEA? Arsenal itapambana na Bayern Munich katikati ya wiki kwenye mchezo wa Champions League hatua ya makundi - mchezo ambao wanatakiwa kushinda - kabla ya kuwakaribisha Everton wikiendi ijayo. Watford, ambao wameshuka hadi nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Premier League, watakuwa wageni wa Stoke.

No comments:

Post a Comment