karibu

kwa habari moto moto

Friday, March 18, 2016

mbowe na uteuzi wake

Mwenyekiti wa chadema mheshimiwa Freeman Mbowe kafanya yale aliyo yafanya Dk John pombe magufuli katika uteuzi wake wa katibu mkuu.

kwanini na thubutu kusema hayo labda turudi nyuma  baada ya kuchaguliwa kuiongoza nchii hii kwa awamu ya tano dk John pombe magufuli kitu ambacho watu walitegemea kuteua waziri mkuu ambae wote walijua Mh Herison mwakyembe  hili halina ubishi ndani yake

kila mtu alikuwa na matumaini makubwa kuwa mwakyembe kutokana na kasi yake  wangeendana na magufuli 

kwa mshangao na hali isiyo tarajiwa magufuli amemteua mh Kassim Majaliwa kuwa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,  sio kwamba majaliwa hakuwa ana fahamika la hasha majaliwa alikuwa anafahamika ila wengi hawakudhani atakuwa waziri mkuu hata kwa 1% kasi yake na utawala wake baada ya kupewa nafasi hiyo watu tunaiona sasa

turejee katika mada kuu usiku wa kuamkia jumapili baraza kuu la chadema lilikuwa na kikao kizito ambacho ilikuwa ina mtafuta mtu ambae ata vaa viatu vya dk wilbroad slaa ambae aliachia ngazi kipindi cha uchaguzi mkuu 2015 baada ya kutofautiana na washirika wenzake mara baada ya kumkaribisha Edward lowasa na kumsimamisha kuwa mgombea wa chadema na ukawa 

Mbowe naye ikampata ya magufuli alikuwa na changa moto hiyo ya kumchagua katibu mkuu naaminimajina yalikuwa mengi na labda watu walikuwa na hisia tofauti na huyu akie chaguliwa, nilipata kusikia watu wengine wakisema mh LISSU wengine Salim mwalim lakini yote kapuni

bila ya uoga mh vicent masinji amechaguliwa kuwa katibu mkuu wa chama hiko ambae nae hakuwa anatajwa na wengi na watu hawakutarajia kama masinji atakuwa katibu mkuu

hii ina msaidia mbowe kutopata maswali mengi  kutoka kwa waandishi mbali mbali kutokana na  ushujaa huu wa kuchagua mtu asiye fahamika baadae anafanya kazi ambayo wengi inakuwa kama mshangao kama ilivyo kwa majaliwa

hii sasa inakomesha dhana ya mapendekezo ya watu pasipo ufuatiliaji kuwa nani anafaa na anaweza endesha sisa katika mlengo wa maendeleo

binafsi mimi mtoa makala simfaham sana lakini hii ya kutushtukiza ina leta tija kuliko hii tulie zoea. sijajua kama ndio sisa inakua au vipi jibu unalo wewe .

kikubwa na heri tuombe amani ya nchi yetu ili isiingie machafuko tuweze kuona mengi ambayo hatukuweza kuyaona katika vipindi vilivyo pita.

oprah ilinipa umarufu -irine uwoya

Msanii wa filamu za Tanzania Bongo movie IRENE UWOYA ameweka wazi wakati anaanza sanaa wazazi wake hawakuwa kutaka afanye kazi hiyo.

Uwoya filamu yake ya awali ilikuwa inaitwa 'DIVISION OF LOVE' kabla ya kufanya OPRAH ambayo imempa umaarufu mkubwa katika filamu hiyo ambayo wapinzani wakubwa kipindi hiko Ray kigos na Steven kanumba walikuwepo katika filam hiyo.ameyasema hayo e.fm kipindi cha uhondo.

Uwoya ambae ana mtoto mmoja aitwaye Crishna amesema filamu hiyo ilimfanya apate mafanikio na hata mme wake ambae amezaa mtoto Suleimani Ndikumana alimueleza kuwa hiyo movie ndio sababu ya kumpenda hadi kumuoa.

amewaasa wasanii wachanga haswa wakike kuwa wabunifu hata wakiwa katika tasnia hii wajaribu kuwa wabunifu ili wapate nafanikio zaidi. 

kuhusu uhusiano na msami amesema  kwa sasa yupo "single" hana mtu na kuhusu ndikumana ameomgeza kuwa hawajaachana kwani hakuna talaka iliyotoka ila kwa sasa wako mbali

uwoya atakuwa na movie yake inayoitwa kisoda na pia mambo mengine mazuri yanakuja

wenger na mustakabli wake

Arsene Wenger ana nafasi ya kuamua  kuwa timu yake iweje ili kama bado anahitaji kubaki emirate na kuwafanya mashabiki zake kupata amani kama ilivyo kwa timu nyingine

nathubutu kusema hayo kwakukiona kikosi cha arsenal na nikilinganisha kipindi barcelona wana pita katika kipindi kama hiki, mwaka 1999 hadi 2003 barcelona hakuweza kuchukua kikombe chochote miaka hiyo walikuwa wana pigania timu yao iweje 
japo nyakati zinatofautiana maana arsenal asipo pata taji lolote msimu huu itakuwa msimu wake wa 12 bila ya kuchukua kombe kubwa

arsenal sio mbaya lakini kuna vitu vingi vinakosekana pale wachambuzi wengi waliitabiria mafanikio makubwa arsenal msimu huu lakini haikuwa hivyo maana sasa kombe lililo baki ni epl ambalo amepitwa alama 12 na kinara wa ligi hiyo Leicester city. 
wenger anaweza kuamua kuwa atumie pesa zilizopo ili arudishe heshima iliyokuwa zamani ukilinganisha kikosi kile ambacho hakikufungwa msimu wa 2003-2004 ''unbeaten'' na ukilinganisha na hiki kilicho pambana na barcelona utaona utofauti 
kikosi hiki hakina watu kabisa una mtanguliza olivier Giroud ambae thiery henry alisha sema wenger huwezi chukua ubingwa ukiwa na Giroud. Hii inaonekana dhahiri kabisa ukosefu wa mmaliziaji ndio tatizo la arsenal msimu huu 
barcelona japo wana watu watatu wakubwa ambao wanaweza kuleta matokeo muda wowote lakini pia wana fungika, Danny welbeck amekosa nafasi mbili za wazi na theo walcot amekosa moja ya wazi ambapo kama zile nafasi angeipata aguero,cavan,lewandowsk au diego costa tungeona matokeo yana badilika pengije hata arsenal ingeweza kupita hatua inayofuata lakini ukosefu wa utulivu na thamani ya washambuliaji wa arsenal inawakosesha nafasi ambayo ilikuwa adimu kwa miaka mitano.
WENGER AFANYEJE?
wenger kama ana hitaji kubaki na kuendelea kutesa ina muhitaji achukue fungu la pesa kisha asafishe sehemu ya mbele yote ya arsenal, olivier giroud ,theo walcot, ,arteta,flamini chamberlen,rosicky na per metersacker wote inatakiwa watumbuliwe majipu. na na achukue watu ambao wataweza kumletea heshima ambayo kaipoteza kwa miaka 12.
achukue nani nani hapo sasa nadhani kila mtu anaweza kuchangia kuwa viwango vya kidunia mfano wa lewandowsk,isco, na aubamayang huo mfano tu ambapo wataweza kubadili arsenal kutoka kudhalauliwa hadi kuheshimika kuna vitu vingi vimekosekana arsenal haswa ushambuliaji.

NINI KINA ITAFUNA ARSENAL
kikubwa kinacho itafuna arsenal morali na kiongozi mkali anaye weza kuongea na wachezaji kwa ukali pia kwa upole kwa hamasa walie iamsha na barcelona hatua ya pili ile ndio wanatakiwa waende nayo hadi ligi kuu sasa hakuna wakuweza kuwa fokea pindi  wanapo zembea pia kocha dhaifu Ferguson mara nyingi kama mlicheza vibaya ndani ya uwanja mtakuja kukiona katika vyumba vya kubadilishia nguo hii wenger hana kabisa ambayo pia ni muhimu kwa kiongozi. 

USHAURI
pia kama hataki kubadili falsafa yake njia rahisi anaweza kuondoka tu ili atoe nafasi kwa wengine lakini bado simtoi miongoni mwa makocha bora barani  ulaya 

lugha chafu hazitakiwai katika michezo

Mkuu wa kitengo cha habari wa timu ya simba Haji Manara amewataka wa Tanzania kuacha kejeli za kudharau kaya au kabila fulani wakati wa kutoa matamshi yao.

hayo ameyasema wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha michezo cha asubuhi cha e.fm kinachoendeshwa na omary Katanga.

hayo yamekuja mara baada ya muda Jeri Muro kulisema kabila la Kizaramo ambali ndio kabila lake Haji Manara ambae ametanabaisha kuwa kabila hilo ndilo lililo anzisha yanga na simba, Yanga1935 na 1936 kwa Simba.

ushabiki na utani wa jadi utabakia pale pale wala hauwezi kuisha ila sio kutoa thamani ya utu hali ya kuwa jioni wanakaa wote kaitka vijiwe vya kahawa.

pia Haji hakubaliani na Tff kuwa achia viporo vingi yanga na azam ambao walikuwa katika michezo ya kimataifa. hadi sasa yanga ana viporo 2 azam 2 .

kabla ya kumaliza mahojiano hayo manara amewaomba waandishi wa habari atakuwa na taarifa kwa vyombo vya habari . 

Tuesday, February 16, 2016

wasanii wa vichekesho inatakiwa wajiongeze,alikiba ni msanii aliye jitosheleza dimond mfanya biashara-KITALE

Wasanii wengi wa sanaa ya vichekesho hawa ji brand bado  wako kama bidhaa maana kuna bidhaa na  brand hayao ni maneno ya mkude simba au kitale na jina aliyo jingine bwakila
akizungunza na kipindi cha mkasi kinacho rushwa na salama jabir mkude ameeleza jinsi wasanii wanatakiwa wanjiongeze ili waweze kunufaika zaidi waongeze ubunifu ili sanaa ya vichekesho izidi kukua alipo ulizwa kuhusu yeye na wasaniiwenigne amesema kuwa yeye ni brand ambayo ina jiongeza  hivyo wasanii ina bidi wakune vichwa

alikiba ni msanii aliye jikamilisha  dimond ni mfanya  biashara  ukikaa na watu wanae jua muziki utaweza kuelezwa vingi na utofauti  ya hawa wasanii alikiba na dimond hawana bifu bifu ina tengenezwa na mashabiki,, alikiba akienda kigoma anashuka ana niacha morogoro yeye anaendelea  ana wakubali wote ila alikiba ni msanii na dimond mfanya biashara
ameongeza kuwa kabila la waruguru ni wabishi mno na ndio maana ame tumia sanaa yake kuweza kuelezea japo sio kwa ubaya
pia ameeleza JOTI,MPOKI NA MZEE MAJUTO ndio haswa ana wakubali  na anatamani waje kufanya kitu kikali kama ikitokea

Friday, February 12, 2016

shetta acha kutumia jina la mamba mara moja-dudubaya

Msanii dudu baya ame ongea na team tz na mwandishi aitwaye emanuel amemwambia kuwa shetta aaache mara moja kutumia jina la Mambo vinginevyo yale yaliyo mkuta mr nice ndiyo yatakayo tokea kwake mkali huyo wa zamani alie hit na ngoma zake miaka ya 2000 ame muasa shetta kuacha maaroa moja kutmia mamba ili awe salama maana msanii huyo anae sifika kwa ugomvi miaka ya katikakti ya 2003 ali mpiga mr nice na kesi yake kudumu miezi sita mahakamani


shetta nae amesikia katika media akitumia jina hilo la mamba kumbuka siku hizi za karibuni kumetokea na ugomvi wa kugombania majina ili make headline pale dimond alipo tumia jina la simba ambao jina hilo la afande sele mr blue kaja juu na ikawa gunzo mitandaoni hivi sasa imerudi kwa sheta naye kutumia jina hilo la mambo dudu baya amejitokeza tena kaongeza a.k.a nyingie ya kujiita oil chafu
makli huyo wa hit song ya nakupenda amesema juma tatu hii ataweka ngoama yake mpya mkito na leo itaanza kusikika club ngoma yake

Thursday, February 11, 2016

nitafanya collabo na alikiba pia christian bella popote alipo namtafuta-seyi shay

shey shay ni msanii wa nigeria amepata umaarufu kwa nyimbo yake ambae ame shuti na @mejialabu wimbo unaitwa right now sasa ametua Tanzania katika show ya mwanza jembe ni jembe ambayo inafayika mwanza valentine day hii shey shay amesema mengi haswa alivyo tua uwanja wa ndege wa julias nyerere millard ayo ndio wa kwanza kumnasa kikubwa maezungunzia show pamoja na mambo mengine ya kimuziki hii itakuwa habari nzuri kwa muziki wa Tanzania msanii huyu ametananbaisha

SEYI SHAY AKIWA KATIKA POZI LA PICHA

kuwa atafanya collabo na ALIKIBA pia ben paul alipo fika katika kipindi cha xxl kinacho endeshwa na bdozen shey sey amesema ana mkubali alikiba japo pia dimond japo hana masawasiliano nae pia amewaomba watangazaji hao wamtafutwe christian bella popote alipo anataka kufanya nae collabo hiyo ameisema wazi yoyote atakae sikia  amwambie ndipo bidozen amesema watawasilisha ombi hilo kwa king of melody christian bella
kumbuka @mejialab amefanya video kali kama ya wizdkid,alikiba chekecha na nyingine nyingi

Tuesday, February 9, 2016

Alikiba-njoo tarehe 14 ununio hawai mmuone baby number one wangu katika valentine day

alikiba akiongea na clouds fm katika kipind cha leo tena amesema siku ya  tarehe 14,02,2014  ata kuja na baby wake siku hiyo ili waweze kumjua maana watu wana hamu ya kumjua, kiba amesema kuwa baby number one wake anamsaidia vitu vingi haswa akipata strees za watu pia mitandao ya kijamii yeye huwa ana mpooza na ana mshauri vitu vingi sana


alikiba akifanya tour yake ya lupela ambayo ndiyo hitsong yake alie itoa hivi karibuni pia amefanya mahojiano na djtas wa magic fm alipo muuliza kuwa naomba uchague muziki mmoja wa dimond akauchagua je utanipenda  kwa kuonesha kuwa ana sikiliza miziki na ngoma kali za wasanii wote
hit maker huyo wa chekecha  mwana na hivi sasa lupela mabapo ni nyimbo tatu tangu arudi miaka miwili iliyo pita na nyimbo moja ya kushirikiana ametanabaisha kuwa collabo ziko baadhi amefanya na nyingine zina kuja ila collabo itakayo fuata itakuwa na sauti sol
dj tasi pia alimuuliza kuhusu ne-yo  akasema vitu vyake vitakuwa suprize kwahiyo wasubiri mwaka huu vitu vizuri vitakuja

Saturday, February 6, 2016

Nilikuwa naficha uhalaza wangu sasa mambo wazi-Neyo

huu ndio muonekano wa neyo ambao siku nyingi alificha muonekano wake  baada ya kusema kuwa kila kitu kina wakati wake

wengi tulifahamu kuwa ile ilikuwa ni fasheni kumbe alikuwa ana ficha uhalaza wake

moja ya picha zilizoko mtandaoni, supertstar huyo ambae alikuja katika project ya coke studio akifanya kazi na alikiba pia kufanya collabo na dimond amepiga picha  akiwa na mke wake akionekana ana ujauzito sasa ndio habari iliyo tazamwa zaidi mitandaoni


Monday, February 1, 2016

arsenal itakumbushia fainali ya 2014 ya fa itakutana na Hull city raundi ya tano kombe la chama cha soka uingereza FA


mabingwa watetezi kombe la fa watakutana na hull city hii kama fainali ya fa 2014 ambapo arsenal walichukua lakini  mechi kali manchester united dhidi ya chelsea
ratiba kamili kama hivi
Araenal vs gull city
Manchester uniited vs Chelsea
tottenham spurs vs crystal palace
liverpool au westham  vs  blackburn
reading vs westbrom au paterborough

lupela kutoka february 4, 2016-alikiba

star wa muziki wa bongo flava na ngoma kama my everything, mwana,chekecha,mali yangu, nagharamia alikiba anatarajia kutoa video yake na audio ya nyimbo yake ya lupela ambayo itakuwa tayari tarehe 4 mwezi huu 02 ,2016 siku ya alhamisi ambapo mashabiki wake wapo na hamu kuweza

kuiona video hiyo ambayo  video quen ni Aaliyah_janey wa usa na director kevin donavon mkongwe pale hollwood

Saturday, January 30, 2016

wasanii wengi hawa kuwa wana mkubali kwa chuki zao kwa kuwa alikuwa ana ng`ara kila kukicha sharo millionea- KITALE

Musa yusuphu mahenge ama kwa jina lililopo katika headline hapa mjini kitale  amesema mengi kuhusu maisha yake ya sasa na filamu yake mpya ambae imetoka hivi karibuni ya shobo dundo ambae ameigiza na rafiki yake wa karibu hivi sasa stan bakora
kitale amesema marehemu sharo milionea ilikuwa nyota ambae kila siku ya  mungu ilikuwa ina waka yaani alikuwa anazidi kimarika kila kukicha hali hiyo imemfanya  wasanii wenzake wamchukie na kutaka kumshikia mapanga kumuua

kitale amesema kuwa wakati wapo mbeya kwa ajili ya kuigiza igizo jipya masele alimshikia panga na kutaka kuupiga nalo kichwani hivyo alifanya jitihada za kumuondoa na usiku wake wakajiengua na kuondoka kambini hapo ndipo wakakutana na ostaz juma na musoma pale morogoro hotelini
ostaz juma alitaka kujitangaza na pia awatangaze wao kwa alimpa laki nane kwa ajili ya kurekodi ndipo akarekodi  HILI DUEDE NOMA na sharo aka enda kwa c9 akarecord na canal top pamoja na rich mavoko
akiongea na millard ayo kitale amesema alikuwa nae bega kwa bega pia tofauti iliyopo kati ya yeye na mama yake sharo imeisha mara baada ya mzazi huyo kutangaza kuwa kuna baadhi ya mali ali baki nazo  kitale wakati huo huo kitale aliorodhesha mali zote na kumpatia mama yake marehemu na kitale amegundua kuwa aliye kuwa ana mjaza manenno mama sharo mtu mwingine lakini wamesha yamaliza
pia kitale aliongeza walikuwa na malengo makubwa na siku moja shalo alimueleza kuwa tufanye kazi wasio nikubali waje kunifuata kitale amesema kuwa chanzo cha chuki hizo na wasanii wenzake ni kupata kujulikana kila siku kukicha
ikumbukwe kuwa sharo milionea kabla ya umauti aliimba nyimbo na dully skies , alikiba,rich mavoko,canal top na nyimbo zote zikawa gunzo mjini either alizo pata kuzitolea video ni ya dully na rich mavoko
kitale ameongezea kuwa hata baada ya msiba wake wasanii wengi ambao walikuwa wote  hawa kuweza kuja

Monday, January 25, 2016

SINA UTAJIRI HUO WA KUFANYA NICHOME MOTO GARI YANGU KWA AJILI YA ARSENAL.madee

ametoa ufafanuzi kuhusu ahadi yake ya kuchoma gari lake mara baada ya kuahidi kabla ya mechi kuwa endapo arsenal ikifungwa na chelsea ata choma gari yake moja ambayo ataiweka manzese watu waje waichome hayo ameyasema shaffihdauda.com baada ya mechi kuisha arsenal ikifungwa goli 1-0 lililo fungwa na diego costa ambae amemsababishia kadi nyekundi nahodha msaidizi wa arsenal per metersacker

madee amesema kuwa ile ilikuwa aweke tention kwa mashabiki wa mpira Tanzania pia watu wengi walikuwa wana utaazama huo mchezo kupitia tension aliyo iweka na ameongeza kuwa hawezi kuchoma moto gari yake maana hana utajiri huo na hata kama angekuwa na utajiri kiasi gani asinge weza kuku furu hivyo
madee ni mmoja wa mastaa wanae ipenda sana arsenal na mfuatiliaji mzuri wa mpira ukiachana na madee  mastaa wengine wanae ipenda arsenal ni Roma mkatoliki,abdul kiba na WENGINE WENGI
arsenal imefungwa mechi zote mbili nyumbani na ugenini
wakati huo huo metheu flamini amevunja rekodi yake mara baada ya kucheza mechi 54 katika dimba la emirate bila ya kufungwa yaani mechi ambazo alizo anza yeye kwa mechi zote jana ni mechi ya 56kwa mtiririko mechi 56 ushindi mechi 36 draw 16 na kufungwa moja

Saturday, January 23, 2016

vazi la kijeshi lina maana kubwa

Raisi wa awamu ya tano wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa dkt John pombe magufuli ni rais wa kwanza  ja ya nchi hii kuvaa nguo au gwanda za kijeshi unaweza kujiuliza kwa watu wa zamani kuwa mbona baba wa taifa alivaa hizi wakati wa vita ya uganda na Tanzania,utofauti uliopo ni kwamba
magwanda yaliyo tumika kwa mwalimu julius kambarage nyerer  haya kuwa na vyeo, Aidha jeshi ni taasisi ambayo imejengwa kwenye mfumo,sgeria,miongozo na taratibu imara ambazo hazipaswi kuingiliana na mifumo ya kisiasa izingatiwe kuwa vyeo  ni lazima vitokane na mafunzo na  elimu pia utumishi husika
jibu liko hapa raisi mteule wa awamu ya nne alikuwa ni mwanajeshi wa cheo cha luteni kanali. hata kama angeamua siku moja kuvaagwanda wala asingeweza kuvaa kwa cheo chake bali ange vaa plan mfano halisi angali hata raisi wa kenya huwa ana vaa plan yaani ange vaa plan kwa hadhi yake ya ukuu wa nchi na majeshi ya ulinzi na usalama
Aidha uvaaji wa gwanda za jeshi ni jambo la kisheria hivyo lilazimishe masharti endapo mkuu wa nchi anataka kulitumia
kwa nchi yetu jeshi letu halijawahi kubuni cheo cha Amiri jeshi mkuu kwa kuwa kimafunzo na kitaratibu cheo kikuu cha mwisho ndani ya jeshi letu ni General. yawezekana gwanda alilovaa uhuru kenyata  ni ile tafsiri yake ni cheo cha FIELD MARSHALL ambacho kwa taratibu za kijeshi hutunukiwa baada ya kupigana vita ambacho kwa taratibu za kijeshi hutunukiwa baada ya baada ya kuwa amepiganisha vita nyingi na amepiganisha vita vingi na kushinda wa utaalam au medani za kivita kwa utaratibu za za kijeshi vazi la kenyatta ni kituko
Tukumbuke   yoweri museni ni mwqana jeshi wa cheo cha ujeneral  hivyo kwake kwake kuvaa gwanda ni sahihi kwa cheo hiko na kupigiwa saluti kwa cheo chake cha Amiri jeshi mkuu na siyo vyeo alivyovaa
mfumo wa jeshi haupigi saluti vyeo au gwanda bali mtu na hadhi yake kwa cheo chake ndiyo maana  mwanajeshi wa cheo fulani huendelea kupigiwa saluti hata pale hayupo katika uniform za kijeshi
 katika hili tumejisfunza mengi kuhusu uvaaji wa hizi sare maalumu na muhimu katika jeshi pia tuangalie sio kila kitu kinacho fanywa na wenzetu ni sahihi au tuige hapana

fanya hayo ili mungu akuongoze katika njia iliyo nyooka



dunia huwa inatukimbiza sana wanadamu mungu tuna muweka mbali sana dini ya uslam ina huwisha yote ambayo binadamu inatakiwa afanye ili apate neema duniani hadi kabrini  ama kwa hakika ukifanya hivi kwa nia mungu atakuongoza
naomba mungu atuongoze katika njia iliyo nyooka insha Allah

Monday, January 18, 2016

at ampa maneno ya shuktani alikiba

Mwimbaji maarufu wa miduara, AT kutoka visiwani Zanzibar amemuandikia Ali Kiba ujumbe wa wazi ambao umefichua baadhi ya mambo kati yao ambayo yalikuwa kapuni. Kupitia mtandao wa Instagram,

 AT ameandika ujumbe huu kwa Ali Kiba: "My dear Brother imekua desturi ya watu kutokumbuka fadhila haya ni ya kwangu binafsi wala hayahusiani na ushabiki usiojenga heshma kwa mtu acha nikutumie barua ya wazi kwako mwaka 2006 mwishoni nilibahatika ulikua shabiki mkubwa wa wimbo wangu wa UTAONA NOMA uliniambia hayo wakati tulipokutana kwa mara ya kwanza wakati nikiwa bado mgeni 

wa jiji la Dar maeneo ya kariakoo mtaa wa Pemba kwa Dada Rahma Mama Swalekh na tukiishi km ndugu hapo wakati ukihit na wimbo wako wa Sinderela mtu wa kwanza kwanza kukupandisha Daladala ni Mimi ‪#‎Ahsante‬ sana kwa heshma ulionipa hata pale ilipofikia nilikuambia naacha muziki uliumua na ukaniambia upo tayari kutoa pesa mfukoni unisaidie na ukanifariji kua nitafanikiwa tu #Ahsante kwa mara ya 2 tuliishi ndugu hadi kwa wazee wetu nilifurahi zaidi kuona ushirikiano wa familia yako ktk harusi yangu misiba na matembezi sikujua hata mm siku nitakua nkombozi kwako baada ya pale kituo cha tv fulani kugoma kupiga video zako eti ya kwamba unadharau niliumia vile haupo ivyo ila show yangu ya zanzibar uzinduzi wangu ukasababisha tofauti hiyo ifutike na ukawa huru zaidi na kufanya video na mtu ambae ilikua akidhani unamaringo na hatimaye ulifanya show hiyo na ulikataa nisikulipe #Ahsante sana uliweza kuniletea Marlow studio wakati akiwa anahit mno nakufanya nae Colabo hadi leo uwowimbo haujachuja hadhi nilijua ww ni mtu wa imani baada ya Msanii fulani wakati tupo Oman mwaka 2010 alikukera sana hadi ulitaka kumpiga ila niliposimama kati huruma ikakujaa hali ya kwamba ulikosewa Ombi langu kwako Ingawa ni mipango ya ‪#‎Mungu‬ ila Unamchango mkubwa mpaka mimi kua ‪#‎AT‬ naomba kati ya Tunzo mbili nilizopata Tanzania Moja nikutunukie ww Moja iyende kwa Adam Juma Good bls you @officialalikiba @adamjuma ( kuna kitu kiba ulikua unakitafuta sana hujafanikiwa kukipata ila kwa kuthamini mchango wako ni kidogo ila kitakufurahisha sana na huenda kikakutoa 
mchozi nakutumia now katika Whatsup yako be happy my Bro SALUTI )(#AT na ‪#‎Alikiba‬ tumefanya jumla ya colabo 3 ya 1 ‪#‎Kwanini‬ ft ‪#‎QeenDarlin‬ ya 2 ‪#‎Usikomae‬#nae na ya3 ni ‪#‎Acha‬#liwachome ila 2 zimesikika moja ni nyimbo anayoipenda mama yangu hamtaisikia mnisamehe ni zawadi 4 my ‪#‎Mumy‬

MWANDISHI NGOSWE KITOVU CHA UZEMBE AFARIKI DUNIA

Edwin senzaba ni mhadhiri chuo kikuu cha dar es salaam lakini pia ni maarufu kwa kitabu chake cha NGOSWE KITOVU CHA UZEMBE  ambayo kilipendwa na kinaendlea kupendwa  nchhini na hata nchi za karibuni mwa tanzania


ngoswe kitovu cha uzembe kina zungunzia maisha ya kawaida na ya kila siku ya mwanadamu na udhaifu wake ambavyo kitabu hiko kina tumika kujibia maswali ya somo la kiswahili kidato cha nne



ney wa mitego sio mwana hip hop-fid q

Fid q ametanabaisha kuwa kwa sasa wanafikiria kuiondoa bongo hip hop katika bongo flava ili ijulikane kuwa nani nanani anae fanya vizuri katika tasnia hiyo akizungunza na clouds fm kipindi cha xxl kipegele cha 255 fi q amesema kuna wasanii ambao wapo kaatika hip hop yaani wana rap ila hawafanyi hiphop mfano amemtaja ney kuwa sio mwana hiphop ila anarap
fid q amewataja baadhi ya watu wa hip hop kuwa young killer ,joy moe stamina, country boy na wengine ila ney wa mitego si mwana hip hop bali ni rap maana unaweza ukarap ila ukawa sio mwana hip hop


wakati huo huo adam mchomvu ameulizwa swala hilo yeye amejibu kuwa ney wa mitego sio mwana hip hop na kuanzia leo anatolewa rasmi katika categories ya hip hop

Saturday, January 16, 2016

TCRA IMEVIFUNGIA VITUO VYA RADIO NA TV KWA KUTOLIPA KODI

Tcra imeifungia radio hizi kwa kutolipa kodi  SAA usiku ndipo utafungwa rasm hadi watakapo lipa kodi
TCRA yavifungia vituo 21 vya Radio na 6 vya Television kwa muda wa miezi 3 kuanzia Jumatatu tarehe 18.
1. Sibuka fm
2. breez fm
3. Country fm
4. Ebony fm
5. Hot fm
6. Impact fm
7. Iringa manicipal Tv
8. Kiss fm
9. Kitulo fm
10. Kifimbo fm
11. Mbeya city municipal Tv
12. Radio 5
13. Radio free Afrika
14. Musa Television network
15. Pride fm radio
16. Radio huruma
17. Radio uhuru
18. Star Tv
19. Rock fm radio
20. Standard fm radio
21. Sumbawanga municipal Tv
22. Tanga City Tv
23. Top radio fm limited
24. Ulanga fm

Friday, January 15, 2016

sio sahihi mtv base kumtumia msanii kujudge kazi za msanii-alikiba

Baada ya kusikika dimond platnumz akijinadi kuwa Mtv wana mpigia simu ili kujaji kazi za wasanii wa bongoflava wakati wakipeleka video zao huko hayo aliya zungunza akiwa na dijaro wa lungu tbc2 katika kipindi cha papaso, clouds fm kupitia xxl kinpengele cha 255 cha perfect chrispin hawakuwa nyuma katika  hilo wakampandia hewani alikiba kueleza alicho sikia hicho kutoka kwa dimond amabapo dimond alisema kuwa yeye sio mbanaji maana kuna conection nyingi amewapa wasanii ikiwemo hiyo ya kuto wabania pindi apigiwapo simu kuhusu kuikubali video ya msanii kutoka Tanzania

alikiba amewataka mtv kutoendelea na hivyo wanavyo fanya au kama kama kweli wana fanya hivyo wanakosea kwa sababu kipaji cha msanii haki jajiwi na msanii mwingine kipaji cha msanii kina jajiwa na fans na wadau wa muziki hivyo kama mtv wanafanya hivyo sio sahihi kabisa kingkiba amesema ila hilo inawezekana kabisa ikawa sio kweli kutokana alilo lisema dimond na akasema 

bongo wanabana location-hanscana

Muongaji wa video ya nasema nawewe ya dimond platnumz Hanscana amesema kinacho wafanya wasanii kutoka nje kwenda south africa  kutoa video kwa sababu ya location hapa bongo location zipo ila watu wanao hitajika watoe hizo location wanakataa director huyo ame itaka serikali ya dr john pombe magufuli kuingilia kati swala hilo ili hata watanzania waweze kuonesha vivutio vyao
hanscana ameongeza kuwa  wasanii wanaenda bondeni kwa ajili ya location na location yenyewe hotel wakati huo huo hotel zipo bongo tena nzuri na wakienda huko wana lipia kama milioni nne hivi sasa kama wamiliki wa hotel tanzania wakikubali hiyo pesa si wana nufaika wenyewe
ameongeza kuwa inabidi serikali hii iweke kifungu kabisa kama wata kataa wamiliki wa hotel wafungwa hayo ameyasema katika kipindi cha xxl kupita 255 ya perfect chrispin

hanscana akiwa moja ya harakati zake nyuma dimond kulia tudi thomas

Monday, January 11, 2016

Tff na serikali hawana makosa juu ya kurejea kwa samata-shaffih dauda

Mchambuzi wa maswala ya michezo Tanzania na pia mfanya kazi wa clouds media group shaffih dauda ame waasa wa Tanzania  kutoandika na kuongea vitu ambayo bado hawaja vifanyia uchunguzi akizungunza katika sports bar ya clouds fm  dauda amesema  mambo yasingekuwa rahisi hivyo kubadilisha tiketi ili afike mchana watu wampokee samata hii inatokana na mashirika yanayo endesha utaratibu wa safari za Tanzania ni mbili ambazo ni kenya air way na ethiopia airline hivyo isinge kuwa rahisi kubadilisha utaratibu ghafla kama watanzania walivyo taka
dauda ameongeza kuwa jitihada zimefanyika ili kuweza kufanya hivyo kwani raisi wa tff  Jamal Malinzi alijaribu kuwa siliana na mwakilishi wake alie ambatana na samata katika safari hiyo ambayo nyota wa tp mazembe mbwana samata ameibuka kuwa mchezaji bora wa afrika anae cheza ligi za ndani na kumuacha rafiki yake robert kidiaba

ametoa mfano wa sisi waandishi wa habari kuwa katika somo la journalism kuna kipengele kina itwa no research no write kama huja fanya uchunguzi usiandike habari hii inatokana na sasa mitandao ya kijamii kuwa mingi na watu kuandika bila kujali na kujua nini kimetokea amewaomba watu wa mitandao ya kijamii kuwa wastarabu na hbari zao ili kusiwe na simto fahamu na kutoa lawama ambazo hazina msingi katika jambo lolote
dauda pia ameongeza ushindi wa aubamayange kuwa kwake yeye aliuona sahihi hii imetokana na yaya toure kulalamika kuwa haikuwa sahihi mgaboni huyo kupata zawadi hiyo ukilinganisha na mafanikio yake kwa mwaka uliopita

Saturday, January 9, 2016

shilole nae afikisha wafuasi milion moja instagramu huku akiachana na nuhu

moja ya vitu vinavyo vutia siku hizi ni mtndao wa instagran wakati wakenya wakiomba wa tanzania tufungiwe katika mtandao huo huku watanzania tukiona kuwadharau na kuwa bussy na zawadi nyingi kutoka katika wasani na wana michezo hivi karibuni kulikuwa na mlolongo mrefu wa watu maarufu kupata wafuasi wengi katika mtandao huo wa picha ambapo imekuwa desturi yetu kila mmojawapo akifiksha wafuasi milioni moja tutamtaja safari hii imeangukia kwa shilole

shilole amepata wafuasi milioni moja wiki hii katika account yake ambayo ameandika shishi baby katika kukumbuka tu wa awali kabisa ni dimond platnumz akafuata millard ayo akafuata wema sepetu akaja vanesa mdee akafuatia joketi kidoti  na akaja jackline wolper  na hatimae shilole mtoto wa nzega
amabapo kwa  sasa hayupo tena na Nuh mziwanda hayo ameya tanabaisha kupitia bongo five kuwa  it is over me  na nuhu amesema shilole


magufuli ni musa atakae tuvusha -Mapenzi michael

Miongoni mwa mambo ambayo kwa sasa yanaonekana tofauti ni uongozi huu wa dk john pombe magufuli ambapo kwa kipindi kifupi alicho kaa madarakani amefanya kazi ya miaka mitano iliyo pita ya seriikali iliyo pita hilo halina ubishi kwa watanzania walie mpigia kura na walie mpigia kura ndugu john pombe magufuli kushika hatamu hii hii ya uongozi wa awamu ya tano ya jamhuri ya muungano wa Tanzania
Mapenzi Michael ni moja ya watu walio kuwepo katika kinyang`anyiro cha uchaguzi mkuu ulio fanyika oktoba 25, 2015 na kuamua magufuli kuwa raisi wa nchi hii tulivu ya Tanzinia katika mahojiano na mwandishi wa blog hii mapenzi michael amezungunza mengi kuhusiana na imani yake juu ya serikali hii
Mapenzi michael yeye ni mzaliwa wa dodoma kata ya chamkoroma ambapo alikuwa an pigania achukue hatamu kwa ngazi ya udiwani katika kata ya chamkoroma hapo hapo alipo zaliwa na kushindwa uchaguzi huo na ccm kuchukua ushindi kupitia kwa DIMONI

Mapenzi michael akiwa katika kava wakati anagombea udiwani chamkoroma mkoani dodoma

katika mazungunzo yetu mapenzi ameelezea haswa uwajibikiaji wa john pombe magufuli pia emetoa pongezi kwa kuweza kutekeleza ahadi yake ya elimu bure ambayo tumesikia zimetanganzwa bilion 18.77 ziende shule zote za serikali kwa ajili ya ahadi yake alio itoa kwa elimu bure
amepongeza magufuli kwa kuwa viongozi waliopita hawakuweza kutimiza ahadi zao kwa wakat i tena kuna wengine miaka miwili ya mwisho ya uongozi wao ndio wameanza kutekeleza japo ahadi zao na hazikuika mwisho
akitoa mfano mzuri wa viongozi mapenzi michael amemtolea mfano zito kabwe kuwa  hata akija kugombea jimbo lolote hapa Tanzania mh zitto kabwe ataweza kuchaguliwa kwakuwa ahadi zake anazitekeleza kwa wakati na huwa hafanyi siasa nyingi huwa anatekeleza kile wananchi wanacho kitaka hiindio aina ya viongozi tunao wahitaji
namfananisha magufuli na musa ambae alifanya juhudi ili kuwakomboa ndugu zake na hii inafana na yeye chama alicho kuwa watu wengi hawakuwa na imani kuwa angeweza kutumbua majipu ambapo nafikiri hat angechukua lowasa asinge weza kufanya yote japo mabadiliko yange kuwepo kweli ameongeza mapenzi kuwa alicho kifanya farao ni kama ccm na magufuli ni kama musa   yaani farao aliwachinja watotot wote wakiume baada ya kujua kuwa kuna mtu atakuja kupindua na hii ina fana kabisa na magufuli na anacho kifanya sasa
pia ametanabaisha kuwa endapo ataendelea hivi anavyo fanya hata 2020 ataweza kupata kura nyingi zaidi mana wananchi watakuwa na imani nae na hii ndio haswa upinzania tulikuwa tunataka kuwa tunatka Tanzania mpya ambayo inayo jitegemea na nina amini kwa kasi hii ya ukusanyaji wa mapato bajeti ya mwaka huu itakuwa na mabadiliko makubwa michael amealizia kuwa  hii ndio haswa tulie kuwa tuna itaka

hapa mapenzi akiwa jukwaani akinadi sera
ALIPO MUULIZA KUHUSU VIONGOZI WENGINE WALIO KUWA KATIKA MBIO HIZO mapenzi amejibu kuwa kama nilivyo kueleza haswa mpinzani wake ambae ni lowasa asinge weza kufanya yote hayo kwakuwa na yeye ni mfanya biashara mkubwa sasa kuwazuiya na kuwabana wafanya biashara ni kama na yeye angejibana pia
pia ameongeza kuhusu watu kulalamika baraza la mazwaziri kuwa kubwa mapenzi alikuwa  na maoni tofauti ameotoa mfano serikali iliyo piayta ilikuwa na jopo la watu 60 yaani ninusu ya hii alo chagua dk magufuli bado baraza ni dogo mno na alicho angalia magufuli ni kwamba kama kiongozi anauwezo wa kupiga kazi kwanini ajaze wengi pia amewapongeza wengine wakina mwigulu mchemba ,january makamba na kusema kuwa miongoni mwa wachapakazi
alipo ulizwa kuhusu mapungufu ya mh rais kwa kipindi hki bado amesema haja yaona ila tusubiri na tuzidi kuliombea taifa letu lizidi kupata viongozi wa aina hii kwani tuta weza kujongoza wenyewe pia ameomba zanzibar haki itumike na alie shinda atangazwe ili tuzidi kulijenga taifa letu

Friday, January 8, 2016

Aubamayange hakustahili tunzo-YAYA TOURE


YAYA TOURE AKIWA KAZINI MANCHESTER CITY

Mchezaji wa Manchester city na ivory coast Yaya toure ame zilaumu tuzo zilizo tolewa  afrika mwaka huu kipengele alicho kipinga  ni kile alicho kuwa anashindana na pierre aubamanyang cha mchezaji bora anae cheza soka nje ya afrika
kiungo huyu mwenye miaka 32 ameiwezesha kuchukua kombe ivory coast la afrika mwaka uliopita tangu wafanye hivyo mwaka 1992 na alitajwa kuwa katika kikosi bora  ktk mashindani hayo
amepoteza ushindi huo endapo angeshinda ingekuwa rekodi yake ya kipekee maana angechukua mara tano ange mshinda samuel etoo 
yaya toure amesisitiza kuwa hata fifa wkwa uchafu wote tunao usikia ila kwa hili wasinge fanya hivi hata kidogo, shughuli hiyo ya kuchagua mchezaji bora imefanywa na makocha na watu wa ufundi kumchagua mchezaji bora  nimesikitishwa sana na tukio hili yaya akiongea na  AFRIQUE FOOT `` ninasikitisha kuona afrika nayo inafikia hapa tulipo fika hawa fikirii kuwa mafarikio ya afrika ni muhumi sana, nafikiria hii ni aibu kwa bara hili sisi waafrika hatufikirii kuwa afrika ni muhimu sana tunapenda kuiga kila kitu kutoka nje mabapo sio sawa alisema toure,
yaya toure anasifika kuwa husema ukweli wakati swali linapo kuja katika interview zake
mwisho amemalizia kuwa yaya toure ata jihurumia mwneyewe kama yaya toure  na acha afrika ijihudumie kama afrika

MAREKANI WAMTAKA MAGUFULI HARAKA

Wakati baadhi ya Wamarekani wakiendelea kumwangalia Rais Magufuli kwa kutumia jicho la curiosity, awe and wonder kwa kile anachokifanya kwa Tanzania ambacho wengi wanamsema ni totally unAfrican leader for being serious, honest and hardworking in a continent where, in general, corruption and embezzlement of public funds are a way of life for African leaders.
Baadhi ya wanadiplomasia wa Marekani wameanza kumuomba Rais Obama akutane haraka na Rais Magufuli. Mmoja wa Wanadiplomasia hao ni Johnnie Carson ambaye alikuwa US Assistant Secretary of State for African Affairs kutoka mwaka 2009 mpaka 2012.

Carson amemtaka Rais Obama kukutana mapema na Rais Magufuli kwa sababu Marekani ni mshirika wa karibu sana na Tanzania na pia Marekani inaihitaji sana Tanzania katika mipango yake kwenye Nchi za Maziwa Makuu ambazo ni Tanzania, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, na Uganda.

‘’Bila kuihusisha Tanzania kwa ukaribu zaidi, amani haiwezi kupatikana katika nchi za Burundi and the eastern Congo’’ Alisema Carson.

Mwanadiplomasia Carson ambaye kwa sasa ni Senior Advisor at the United States Institute of Peace na pia ni Senior Fellow at the Jackson Institute at Yale University ameenda mbele zaidi na kusema, Marekani inamhitaji sana Rais Magufuli hasa ikichukuliwa kwa vile historia inaonyesha hana uhusiano wa karibu na Marekani ikilinganishwa na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete.

Hii ni sehemu ya andiko lake;

Invite Tanzania’s newly-elected President John Magufuli to the White House.

Tanzania is one of the most populous states and the largest democracy in East Africa. It is also one of the biggest recipients of US development assistance and a participant in all of Washington’s major economic initiatives.

In late October, Tanzania held presidential and parliamentary elections. The elections on the mainland went well, but those on the island of Zanzibar were disputed. John Pombe Magufuli, a reform-minded academic-turned-politician, was elected without dispute, making him Tanzania’s fifth elected president in a row. Although the Zanzibar election remains unresolved, it is important to reach out to Tanzania’s new president early in his tenure to continue to foster the strong relationship between Dar es Salaam and Washington. This is particularly important since Magufuli does not have any major ties with the US.

An early visit to Washington could consolidate the growing economic and development ties between the US and Tanzania and lend encouragement to the continuation of the country’s democratic progress, including finding a sustainable resolution to Zanzibar’s electoral issues.

Tanzania also has a critical role to play in East African peace building issues, particularly in Burundi and the eastern Congo. Early political consultations with Magufuli and his new foreign minister, Dr. Augustine Mahiga, could prove valuable in promoting stability in the Great Lakes 

hii habari nime iko na kupest kutoka MASAMABLOG 

JARIDA LA MAREKANI AFRICAN SUN LAMTAJA KIKWETE RAISI BORA 2015 AFRIKA

Raisi mstaafu wa awamu ya nne wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dr jakaya mrisho kikwete ametajwa kuwa ndiye rais bora barani afrika kwa muongo mmoja ulio pita ,kikwete ametajwa na jarida moja nchini marekani kama kiongozi ambaye amesimamia amani na kufuata democrasia ambayo nchi nyingine barani afrika wameshindwa kutekeleza hayo

kikwete pia amesistizwa kuwa anahitajika sana katika kutatua migogoro iliyopo barani afrika na kushughulikia mambo mengine barani humo

MAELEZO YA JARIDA HILO
Dr. Jakaya Kikwete, former President of the United Republic of Tanzania.  President Kikwete served his country for 10 years of two terms and participated actively in the selection of the successor President John Magufuli, thereby continuing the tradition of democratic governance in Tanzania, in contrast to some of the neighboring countries where Presidents have abrogated the constitution to further their political ambitions.  President has received so many honors for excellence and so many honorary doctorates by many universities.  Africa would continue to need him for the peace negotiations he achieved not only during his presidency, but as well as when he was Tanzania’s foreign minister for 10 years.”

bilion 18.77 zimetolewa shule zote za serikali nchi nzima kwa ahadi ya shule bure msinig hadi kidato cha nne

Raisi john pombe magufuli ameanza kutekeleza agizo na ahadi yake ya kuwa elimu itakuwa bure kuanzia chekechea hadi kidato cha nne kwa wanafunzi wote Tanzania hii aliitoa wakati akiwa katika kampeni za uchaguzi mkuu ambazo zilifanyika  octoba mwaka ulipita na yeye kuibuka mshindi kwa kura milioni 8 dhidi ya milion sita za edward lowasa
akizungunza na waandishi wa habri waziri wa fedha dk phiph mipango ametanabaisha kuwa pesa tayari zisha mwagwa mashuleni na halimashauri zote nchini Tanzania hivyo kutoa fursa kwa wat0t0 kuweza kujisomea bure
hapo awali kulikuwa na simtofahamu baada ya wengi kukosoa ahadi hiyo lakini waziri wa fedha amesema takribani milion 18.77 tayari zimetoka na amewataka waandishi wa habari kusambaza habari hizo kwa shule zote  kubandika kiasi walicho pokea kutoka hailimashauri ili watu wa eneo husika wafahamu kuwa kiasi gani shule yao imepokea

Waziri wa fedha dk PHILIPH MPANGO
Aidha mheshimiwa  dk philiph mpango amesema kuwa  bilion  15 zimetolwea katika shule hizo na bilioni 3 zimetengwa kwa ajili ya wasimamizi wa mitihani ukijumlisha utapata bilioni 18

hongera mbwana samata ila,,,,,,,,,,?

Mbwana Ally Samatta usiku wa kuamkia 08.2016 ulikuwa mzuri kwake na taifa la Tanzania kwa ujumla  bbada ya kuwa shinda wapinzani wake haswa aliye kuwa nae timu moja rebort kidiaba kwa kura 112 kwa 88 za kidiaba ambazo kura hizi hupigwa na makocha na wanachama wa vyama vya soka barani afrika hivyo mbwana samatta kuwa mshindi na kuchukua hatamu hiyo ya kuipeperusha bendera ya tanzania kimataifa katika soka ama kabumbu
Tuna kila sababu ya kushangilia ushindi wake kwani ni mara ya kwanza tunafanya vitu vikubwa kama hivyo kaktika soka ingawaje katika muziki tangu mwaka jana dimond ameipeperusha bendera vizuri sana na kuweka katika ramani
kwanini mbwana samata amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa afrika wanao cheza ligi za ndani hii imetokana na uwezo wake alio jaliwa na mungu pia juhudi binafsi hii ndio sifa kuu ya kijana huyu kuweza kushinda tunzo hii lakini tunashangilia ushindi wa samata pia hatufikirii kuwa tuna taka watu kama samata kama 100 hatuna mipango yoyote ambayo itaweza kutufanya tuwekeze kwa samata kumi au ishirini kwanini isiwe sisi na kwanini tusiwe na mipango kila kitu kinaendana na mipango na juhudi hii ianzie seriakalini kama wanavyo tumbua majipu inatakiwa watumbue majipu ya kwenye mpira pia

tukipata watu wazuri wanao weza kuongoza soka ndipo tuta weza kupata samata wengine kumi kwa sasa kinacho takiwa kuangaliwa ni uendeshwaji wa weledi katika soka hili la kibongo kwanini tusiweze hali yakuwa tuna vipaji vinavyo weza kututoa kimaso maso kwa miaka hataa kumi mfululizo kama tuta wekeza vizuri? sina shaka samata ataitwa na magufuli kumpongeza ikulu na yeye atumie fursa hiyo kumueleza vitu vinavyo husu mpira kama tumeweza kumtoa mmoja japo kwa miaka mingi na safari yake imeanzia mbali tuta shindwaje kuwatoa wengine ambapo vituo vya mpira vimeshajengwa
napata kujiuliza kulikuwa na mpango wa kuwa sajili watoto tuliwaleta wanetu pale karume ile program sijui imeishia wapi? lakini pia hii inatakiwa kujitoa muhanga kwa vina na viongozi kila kitu sasa ni dili unaweza kusema kuwa mpira na muziki kwa sasa kila kitu kimekuwa dili kwa rika zote japo kila kitu kinaendana na wakati wake
thoamsi ulimwengu yeye hakupitia simba wala yanga katika harakati zake amepitia soka la watoto na hii leo ana timua vumbi na anakula mshahara mzito pale tp mazembe vituo kama vile ndivyo tunavyo hitaji ili  tukuze zaidi vijana kama ulimwengu katokea under 17 hadi 21 na kuwa lulu pale tp mazembe na leo hii tetesi zina sema anaenda france kwanini tusi gangamale katika  hili tuchangamkie dili
waziri anae husika au mwenye dhamana ya kushughulikia michezo japo sio mwanamichezo katika uhalisia ila naamini kupitia dk john pombe magufuli raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ataweza kutuvusha hapa tulipo na kutupeleka mbele kwa ksukumo huo ambao mbwa samata ameuonesha
nawaacha na maswali haya
Ushindi wa Mbwana Sammatta.
Tusikae kupiga Makofi na Vigeregere tu, juu ya ushindi wake! Duru ya Soka Tanzania ina cha kujifunza kwake!
Kama ningeulizwa ningejibu hivi.
Soka la Tanzania linahitaji kujiuliza haya:
1-Tumehusika kiasi gani kwenye kukuza kipaji chake.
2-Tunatumiaje nafasi yake kukuza Soka la Nyumbani na vipaji vinavyochipukia.
3-Tumeandaa nini kumpa ngao ya heshima kwa matokeo ya jitihada zake.
4-Tunampa nafasi gani mbali na kuwa mchezaji wa Timu ya Taifa,katika kuchochea maendeleo ya soka Tanzania.
Hayo ni baadhi tu, maswali mengine ongeza mwenyewe.
Mbwana Samatta,Hongera sana.

Tuesday, January 5, 2016

mapacha walio achana mwaka mmoja kwa dk 2

hawa ndo mapacha walio achana mwaka mmoja


 kwa maana mmoja amezaliwa saa tano na dk 59 usiku mwingine saa sita na  dk 1 mwaka unaofuata

yaani wakiume kazaliwa 31.12.2015  23:59 na wakike kazaliwa saa 00:01 01.01,2016

Sunday, January 3, 2016

NIA YANGU KATIKA MICHEZO



NADIR HAROUB...KELVIN YONDAN...AGREY MORIS...umri wao ni mkubwa lakini bado wanaweza cheza mpira hata miaka 7 ijayo
unaweza kujiuliza kwanini nimeropoka hivi... ni kweli mpira wa sasa unahitajika vijana ambao damu changa ambao wanauwezo wa kukimbia na kuendana na kasi ya washambuliaji
point: je kwa Tanzania hii kuna striker gani ambae ataweza kuwachosha hawa mabeki hadi tuseme wamechoka? na umri wao mkubwa? hii ndio sababu kubwa ambayo naweza kusema hata miaka 7 wanaweza cheza kwa mpira wa bongo.
Kwa kawaida nimewachukua mabeki wachache ila wapo wengine ambao timu nyingine wengine viungo lakini hata washambuliaji ila hii leo nita waelezea hawa mabeki kwa kuwa wanapewa lawama kubwa hii ilitokea mara baada ya timu ya taifa Tanzania kufungwa na libya ila hata kabla ya hapo watu wana zungungunzia utayari uliopo kwa nadir haroub ,kelvin yondani  kuwa wamezeeka sasa wawa pishe vijana wakacheze mpira wa ushindani ni sawa kwa soka la kisasa vijana wakichukua hatamu ila tusipende mabadiliko yasiyo na lazima wakati tuna muda wakuweza kuweka mabadiliko yaliyo kuwa na tija ambayo yatazaa faida kwa Taifa na dunia nzima
mabadiliko ynayo hitajika sio mabadiliko ya ghafla ni mabadiliko ya kujipanga na ushauri kwa viongozi wa mpira timu ya taifa hii iendelee wasiivunje kama wachambuzi wengi wa bongo wanavyo taka kinacho hitajika hapo iandaliwe timu ya watoto wenye miaka 14 hadi 16 wakae pamoja kwa zaidi ya miaka 5 naamini kuna vipaji vingi ila sio kuwashambulia waliopo kutokana na soka letu la Tanzania lilivyo 
nadir na yondani ni miongoni mwa mabeki bora Tanzania waliopo katika form na naamini hakuna mshambuliaji wa kuweza kuwa sumbua hadi tuseme wamechoka  utaweza kusema kuwa kipre tchetche,donald ngoma,amis tambwe,hamisi kiiza na wengine wachache ambao si wengi wakuweza kuwasumbua lakini tuwe wa kweli viwango vyao bado si vya kuwa sumbua hawa mabeki ambao nimewataja ndio haswa kiini cha makala hii nilizunguka katika vijiwe mbali mbali nimesikia wakiwalaumu kuwa wamechoka sasa tusikurukpukie maendeleo wakati hatuja jipanga kufanya maendeleo 
maendeleo yana kuja baada ya kujipanga kisawa sawa hivyo hivyo katika mpira timu ikijipanga sawa sawa inachukua ubingwa na itafanya vizuri mfano mzuri TP mazembe na nyingine wamejipanga na matokeo yake ndio kama haya ambayo tuna yaona kikubwa tuwe na uvumilivu  pia  tuwe watu wa ushauri  kwa viongozi walio katika mpira a,bao itaweza kulisaidia soka letu ,