NADIR HAROUB...KELVIN YONDAN...AGREY MORIS...umri wao ni mkubwa lakini bado wanaweza cheza mpira hata miaka 7 ijayo
unaweza kujiuliza kwanini nimeropoka hivi... ni kweli mpira wa sasa unahitajika vijana ambao damu changa ambao wanauwezo wa kukimbia na kuendana na kasi ya washambuliaji
point: je kwa Tanzania hii kuna striker gani ambae ataweza kuwachosha hawa mabeki hadi tuseme wamechoka? na umri wao mkubwa? hii ndio sababu kubwa ambayo naweza kusema hata miaka 7 wanaweza cheza kwa mpira wa bongo.
Kwa kawaida nimewachukua mabeki wachache ila wapo wengine ambao timu nyingine wengine viungo lakini hata washambuliaji ila hii leo nita waelezea hawa mabeki kwa kuwa wanapewa lawama kubwa hii ilitokea mara baada ya timu ya taifa Tanzania kufungwa na libya ila hata kabla ya hapo watu wana zungungunzia utayari uliopo kwa nadir haroub ,kelvin yondani kuwa wamezeeka sasa wawa pishe vijana wakacheze mpira wa ushindani ni sawa kwa soka la kisasa vijana wakichukua hatamu ila tusipende mabadiliko yasiyo na lazima wakati tuna muda wakuweza kuweka mabadiliko yaliyo kuwa na tija ambayo yatazaa faida kwa Taifa na dunia nzima
mabadiliko ynayo hitajika sio mabadiliko ya ghafla ni mabadiliko ya kujipanga na ushauri kwa viongozi wa mpira timu ya taifa hii iendelee wasiivunje kama wachambuzi wengi wa bongo wanavyo taka kinacho hitajika hapo iandaliwe timu ya watoto wenye miaka 14 hadi 16 wakae pamoja kwa zaidi ya miaka 5 naamini kuna vipaji vingi ila sio kuwashambulia waliopo kutokana na soka letu la Tanzania lilivyo
nadir na yondani ni miongoni mwa mabeki bora Tanzania waliopo katika form na naamini hakuna mshambuliaji wa kuweza kuwa sumbua hadi tuseme wamechoka utaweza kusema kuwa kipre tchetche,donald ngoma,amis tambwe,hamisi kiiza na wengine wachache ambao si wengi wakuweza kuwasumbua lakini tuwe wa kweli viwango vyao bado si vya kuwa sumbua hawa mabeki ambao nimewataja ndio haswa kiini cha makala hii nilizunguka katika vijiwe mbali mbali nimesikia wakiwalaumu kuwa wamechoka sasa tusikurukpukie maendeleo wakati hatuja jipanga kufanya maendeleo
maendeleo yana kuja baada ya kujipanga kisawa sawa hivyo hivyo katika mpira timu ikijipanga sawa sawa inachukua ubingwa na itafanya vizuri mfano mzuri TP mazembe na nyingine wamejipanga na matokeo yake ndio kama haya ambayo tuna yaona kikubwa tuwe na uvumilivu pia tuwe watu wa ushauri kwa viongozi walio katika mpira a,bao itaweza kulisaidia soka letu ,
No comments:
Post a Comment