karibu

kwa habari moto moto

Friday, January 8, 2016

hongera mbwana samata ila,,,,,,,,,,?

Mbwana Ally Samatta usiku wa kuamkia 08.2016 ulikuwa mzuri kwake na taifa la Tanzania kwa ujumla  bbada ya kuwa shinda wapinzani wake haswa aliye kuwa nae timu moja rebort kidiaba kwa kura 112 kwa 88 za kidiaba ambazo kura hizi hupigwa na makocha na wanachama wa vyama vya soka barani afrika hivyo mbwana samatta kuwa mshindi na kuchukua hatamu hiyo ya kuipeperusha bendera ya tanzania kimataifa katika soka ama kabumbu
Tuna kila sababu ya kushangilia ushindi wake kwani ni mara ya kwanza tunafanya vitu vikubwa kama hivyo kaktika soka ingawaje katika muziki tangu mwaka jana dimond ameipeperusha bendera vizuri sana na kuweka katika ramani
kwanini mbwana samata amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa afrika wanao cheza ligi za ndani hii imetokana na uwezo wake alio jaliwa na mungu pia juhudi binafsi hii ndio sifa kuu ya kijana huyu kuweza kushinda tunzo hii lakini tunashangilia ushindi wa samata pia hatufikirii kuwa tuna taka watu kama samata kama 100 hatuna mipango yoyote ambayo itaweza kutufanya tuwekeze kwa samata kumi au ishirini kwanini isiwe sisi na kwanini tusiwe na mipango kila kitu kinaendana na mipango na juhudi hii ianzie seriakalini kama wanavyo tumbua majipu inatakiwa watumbue majipu ya kwenye mpira pia

tukipata watu wazuri wanao weza kuongoza soka ndipo tuta weza kupata samata wengine kumi kwa sasa kinacho takiwa kuangaliwa ni uendeshwaji wa weledi katika soka hili la kibongo kwanini tusiweze hali yakuwa tuna vipaji vinavyo weza kututoa kimaso maso kwa miaka hataa kumi mfululizo kama tuta wekeza vizuri? sina shaka samata ataitwa na magufuli kumpongeza ikulu na yeye atumie fursa hiyo kumueleza vitu vinavyo husu mpira kama tumeweza kumtoa mmoja japo kwa miaka mingi na safari yake imeanzia mbali tuta shindwaje kuwatoa wengine ambapo vituo vya mpira vimeshajengwa
napata kujiuliza kulikuwa na mpango wa kuwa sajili watoto tuliwaleta wanetu pale karume ile program sijui imeishia wapi? lakini pia hii inatakiwa kujitoa muhanga kwa vina na viongozi kila kitu sasa ni dili unaweza kusema kuwa mpira na muziki kwa sasa kila kitu kimekuwa dili kwa rika zote japo kila kitu kinaendana na wakati wake
thoamsi ulimwengu yeye hakupitia simba wala yanga katika harakati zake amepitia soka la watoto na hii leo ana timua vumbi na anakula mshahara mzito pale tp mazembe vituo kama vile ndivyo tunavyo hitaji ili  tukuze zaidi vijana kama ulimwengu katokea under 17 hadi 21 na kuwa lulu pale tp mazembe na leo hii tetesi zina sema anaenda france kwanini tusi gangamale katika  hili tuchangamkie dili
waziri anae husika au mwenye dhamana ya kushughulikia michezo japo sio mwanamichezo katika uhalisia ila naamini kupitia dk john pombe magufuli raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ataweza kutuvusha hapa tulipo na kutupeleka mbele kwa ksukumo huo ambao mbwa samata ameuonesha
nawaacha na maswali haya
Ushindi wa Mbwana Sammatta.
Tusikae kupiga Makofi na Vigeregere tu, juu ya ushindi wake! Duru ya Soka Tanzania ina cha kujifunza kwake!
Kama ningeulizwa ningejibu hivi.
Soka la Tanzania linahitaji kujiuliza haya:
1-Tumehusika kiasi gani kwenye kukuza kipaji chake.
2-Tunatumiaje nafasi yake kukuza Soka la Nyumbani na vipaji vinavyochipukia.
3-Tumeandaa nini kumpa ngao ya heshima kwa matokeo ya jitihada zake.
4-Tunampa nafasi gani mbali na kuwa mchezaji wa Timu ya Taifa,katika kuchochea maendeleo ya soka Tanzania.
Hayo ni baadhi tu, maswali mengine ongeza mwenyewe.
Mbwana Samatta,Hongera sana.

No comments:

Post a Comment