karibu

kwa habari moto moto

Friday, March 18, 2016

wenger na mustakabli wake

Arsene Wenger ana nafasi ya kuamua  kuwa timu yake iweje ili kama bado anahitaji kubaki emirate na kuwafanya mashabiki zake kupata amani kama ilivyo kwa timu nyingine

nathubutu kusema hayo kwakukiona kikosi cha arsenal na nikilinganisha kipindi barcelona wana pita katika kipindi kama hiki, mwaka 1999 hadi 2003 barcelona hakuweza kuchukua kikombe chochote miaka hiyo walikuwa wana pigania timu yao iweje 
japo nyakati zinatofautiana maana arsenal asipo pata taji lolote msimu huu itakuwa msimu wake wa 12 bila ya kuchukua kombe kubwa

arsenal sio mbaya lakini kuna vitu vingi vinakosekana pale wachambuzi wengi waliitabiria mafanikio makubwa arsenal msimu huu lakini haikuwa hivyo maana sasa kombe lililo baki ni epl ambalo amepitwa alama 12 na kinara wa ligi hiyo Leicester city. 
wenger anaweza kuamua kuwa atumie pesa zilizopo ili arudishe heshima iliyokuwa zamani ukilinganisha kikosi kile ambacho hakikufungwa msimu wa 2003-2004 ''unbeaten'' na ukilinganisha na hiki kilicho pambana na barcelona utaona utofauti 
kikosi hiki hakina watu kabisa una mtanguliza olivier Giroud ambae thiery henry alisha sema wenger huwezi chukua ubingwa ukiwa na Giroud. Hii inaonekana dhahiri kabisa ukosefu wa mmaliziaji ndio tatizo la arsenal msimu huu 
barcelona japo wana watu watatu wakubwa ambao wanaweza kuleta matokeo muda wowote lakini pia wana fungika, Danny welbeck amekosa nafasi mbili za wazi na theo walcot amekosa moja ya wazi ambapo kama zile nafasi angeipata aguero,cavan,lewandowsk au diego costa tungeona matokeo yana badilika pengije hata arsenal ingeweza kupita hatua inayofuata lakini ukosefu wa utulivu na thamani ya washambuliaji wa arsenal inawakosesha nafasi ambayo ilikuwa adimu kwa miaka mitano.
WENGER AFANYEJE?
wenger kama ana hitaji kubaki na kuendelea kutesa ina muhitaji achukue fungu la pesa kisha asafishe sehemu ya mbele yote ya arsenal, olivier giroud ,theo walcot, ,arteta,flamini chamberlen,rosicky na per metersacker wote inatakiwa watumbuliwe majipu. na na achukue watu ambao wataweza kumletea heshima ambayo kaipoteza kwa miaka 12.
achukue nani nani hapo sasa nadhani kila mtu anaweza kuchangia kuwa viwango vya kidunia mfano wa lewandowsk,isco, na aubamayang huo mfano tu ambapo wataweza kubadili arsenal kutoka kudhalauliwa hadi kuheshimika kuna vitu vingi vimekosekana arsenal haswa ushambuliaji.

NINI KINA ITAFUNA ARSENAL
kikubwa kinacho itafuna arsenal morali na kiongozi mkali anaye weza kuongea na wachezaji kwa ukali pia kwa upole kwa hamasa walie iamsha na barcelona hatua ya pili ile ndio wanatakiwa waende nayo hadi ligi kuu sasa hakuna wakuweza kuwa fokea pindi  wanapo zembea pia kocha dhaifu Ferguson mara nyingi kama mlicheza vibaya ndani ya uwanja mtakuja kukiona katika vyumba vya kubadilishia nguo hii wenger hana kabisa ambayo pia ni muhimu kwa kiongozi. 

USHAURI
pia kama hataki kubadili falsafa yake njia rahisi anaweza kuondoka tu ili atoe nafasi kwa wengine lakini bado simtoi miongoni mwa makocha bora barani  ulaya 

No comments:

Post a Comment