Ne-Yo Arekodi Wimbo na Wasanii wa Barani Afrika Ndani ya Coke Studio Africa Msimu wa 3
Africa inakaribia kushuhudia moja kati ya collabo kubwa zilizowahi kutokea, kupitia Coke Studio Africa! Mkongwe wa R&B na muziki wa Pop NE-YO atashiriki katika msimu huu wa tatu wa Coke Studio Africa.
NE-YO ndio msanii aliyeshirikishwa mwaka huu na atashirikiana na Wangechi (Kenya), Alikiba (Tanzania), Maurice Kirya (Uganda), Dama Do Bling (Mozambique) na Ice Prince (Nigeria) kwa ajili ya hili collabo.

Kabla ya utambulisho wa ngoma hiyo na show, NE-YO alisema “ni jambo la kujivunia kurudi Africa na kushirikiana na wasanii kutoka kote barani. Kwa kuungana na wasanii hawa Coke Studio Africa, watu kutoka mataifa mbali mbali, makabila na dini watakuja pamoja na kuungana kupitia muziki wetu. Nina hamu sana ya kujenga mahusiano na kuweka kumbukumbu na wasanii hawa. "
Miaka 10 iliyopita, NE-YO ametayarisha albamu sita. Albamu yake aliyotoka nayo, In My Own Words ilileta mabadiliko makubwa katika muziki wa R&B ikiwa na ngoma kama “Stay”, “So Sick”, “When You’re Mad” na “Sexy Love”. Albamu yake inayotamba sokoni sasa, Non–Fiction ilitoka January mwaka huu. Albamu hiyo ilishika nafasi ya tano katika US Billboard Top 200, ikimfanya NE-YO mwanamuziki wa kiume wa R&B aliyeweza kuwa na albamu sita mfululizo kuingia katika kumi bora.
Mwaka jana katika msimu wa pili wa Coke Studio Africa, Wyclef Jean aliitumbwiza hit song yake inayofahamika kwa jina la “Divine Sorrow” akiwa na Rabbit, Chidinma pamoja na Shaa. Msimu huu sio wa kukosa!
credit to : coc-cola
credit to : coc-cola
No comments:
Post a Comment