karibu

kwa habari moto moto

Sunday, December 27, 2015

ben paul sio rafiki yangu lakini tuna piga story sana-alikiba

sina ugomvi na ben paoul bali ni washikaji wakawaida ambao tuna piga story za  kawaida wala sina utani na ben paul ila tuko vizuri kwa maana hatuna ugomvi  alikiba amesema yawezekana ameghafirika  maana sikutegemea number yangu anayo angenicheki angeniambia kawaida kwani kila mtu anamawazo yake na anaweza ongea chochote.
ali kiba akiwashukuru mashabiki wake na kuongea mengi na millard ayo tv wakati akiulizwa kuhusu video aliyo enda kufanya marekani alikiba amesema ni video yangu lakini pia nimefanya  tamasha la ile wildaid pia ipo kionjo cha wanyama katika video yangu kama balozi wa wanyama Tanzania nimefanya na nimefanya na director wakubwa ambao wamefanya kazi na wasanii icon (wakubwa duniani)  na  vitu vingi vizuri vitakuja na fans wangu wata furahi

millard alipo muuliza kuhusu account yake ya istagram kama ana mpost mtu anaandika #sorptedbykingkiba alijibu kuwa kila mtu yuko tofauti lakini nataka niwa prove wrong watu ambao wanasema sishrikiani na wenzangu na wajue kuwa nawasapoti na nawathamini
alipo ulizwa kuhusu ushindani uliopo alikiba alikiri kuwa kuna ushindani  mkubwa millard akamuuuliza yeye kitu gani amebadilisha katika ushindani huo akajibu video na hata style ya uimbaji umekuwa mkubwa tofauti na sasa mwimbaji huyu wa mwana na chekecha hivi sasa nagharamia aliyo shirikiana na christian bella amesema hana bifu na mtu yoyote na wala hashindani na mtu yoyotena ameomba upendo katika wasanii ili muziki uzidi kwenda mbali

Saturday, December 26, 2015

ni kweli tunaenda south afrika kufanya biashara nyingine-chege

chege chigunda mtoto wa mama saidi ameweka wazi mipango yake ya kufanya collabo nyingi mwaka 2016 na ametanabaisha kuwa kuna mambo makubwa ya suprize yanakuja mwaka huo akiongea na sam misago wa East africa wa kipindi cha power jam na friday night live pia chege alulizwa na mtangazaji huyo kuhusu neno la afande sele kuhusu wasanii kufanya video south africa


chege amemjibu ni kweli tuna enda kufanya biashara nyingine south africa ameongeza kuwa biashara hiyo ni kutoa video kali ambazo hapo awali hatujawahi kufanya wala hakuna biashara nyingine labda hizo ni ndoto za alinacha kuhisi kuna kitu tauti tunaenda kufanya ,, muziki sasa ni biashara na lazima ujitoe
alipo ulizwa kuhusu kuachana na saidi fella akasema kuwa saidi fela ndio kila kitu hii video aliyo toa sasahivi gharama yote anaijua fella yeye hajui sasa atamuachaje misago alimuuliza tena kuhusu fella na yamotoo chege amesema kwa sasa fella lazima akaae nao wale bado watoto tofauti na wao

Friday, December 25, 2015

Sunday, December 20, 2015

sasa tume waweza wanigeria imebaki 1%

Tumewaweza  hii ndio lugha rahisi ambayo inaweza kutumika katika kuelezea muziki wa Tanzania kwa hatua iliyo fikia  kwa sasa kwanini tumewaweza? Tanzania tuna kila kitu kwa upande wa wasanii wetu ambayo kilicho pungua ni lugha tu kwa maana ya lugha ya kingereza vinginevyo 85% tuko vizuri, kwa sasa tupo nafasi ya kwanza au ya pili tukichuana na nigeria ,
nigeria hawa tuwezi kwa lolote kuanzia mashairi beat na ubora kwa vina lakini kwanini uta shangaa wako juu sana hawa watu  kikubwa walicho kifanya wamewekeza katika muziki kuanzia kupromote nyimbo hadi katika video na kikubwa walicho tuacha sisi ni video ambazo wanafanya uwekezaji mwingi katika hilo
nigeria kama unafuatilia vizuri muziki haswa tumeanza kuwaelewa 2008 na two face idibia ndio baba yao wengi wao hawatoweza kubisha hili kuwa two face ndiye alie itambulisha vizuri nigeria baada ya hapo akaja p-square ndio wakafungua milango mbali mbali kwa wengine kama yule producer jmartins na wengine wakaja wengi wengi wakainua muziki wao  na kuonekana moto wa kuotea mbali walituacha mbali mita 10000 lakini jitihada binafsi  ya mtu mmoja mmoja kama vile dimond platnumz na wengine walio jitahidi  AY , alikiba, muziki wetu sasa umekuwa na kutoka mita elfu kumi sasa tupo karibu yao mita 9999 bado mita moja tu tuwavuke kabisa
hiyo mita moja ina kwamishwa na vitu vifuatavyo lugha,wasanii kutopendana, hawapendi ushirikiano kila mtu mkubwa zaidi ya mwenzake, ubinafsi ,  team hii na timu ile hii ndio mita moja ina kwamisha
wenzetu  wanigeria baada ya kutoboa wakawa wale walie toboa wana peana mashavu wenyewe kwa wenyewe mfano walivyo toka p-square wakawapa mashavu blackets kwa kushirikiana nao baada ya haapo wakashirikiana na jmartins, wakaenda kumpush mr flava mara wakawapush engine na sasa wako juu  na pia uwezo wa mmoja mmoja unaleta changa moto
kwa mashairi yao yanayo tegemea beat kama walivyo south afrika  beat lina wabeba tofauti na sisi beat zuri na mashairi mazuri
kama  watanzania wakiacha ubinafsi kilicho baki kutusua msanii ambae naweza kusema anavyote kwa tanzania ni vanesa mdee huyu ana jua kingereza pia ana jua kiswahili piaa anajua timing ya kumtafuta producer wa beat safi ambaye anaweza kumtengenezea hit song huyu ukinambia heti yemi alade anamshinda nakuwa sikuelewi  yemi alade mashairi yake ya kawaida na mwaka ujao nafikiri vanesa mdee ndiye atakuwa top female in afrika kwa jinsi ilivyo na tuashangaa wote mada ya vmoney itakuja

alikiba ,dimond platnumz,ay,vanesa mdee,belle9,ben paul,lina hawa wanaweza kuwa kuwa manage wasanii wote nigeria isipokuwa p square
kwanini nimesema tume waweza? kwa sasa kilicho baki ilikuwa video bora tu ambayo ushindani uliopo Tanzania kwa sasa  unaleta  faraja watu kutoa vichupa vizuri ambavyo nifaida kwa ajili ya kuwa maliza nigeria sasa tanzania tumeingia katika sehemu ya mwisho ambayo walikuwa wana tufunika katika uwekezaji wa video na sasa tunawekeza video kubwa  mfano video zilizo toka mwezi huu tu ni salamu tosha kwa nigeria, mfano JE UTANIPENDA-hii ina maudhui mazuri sana mle, NAGHARAMIA- ina maelezo mazuri mle katika video , TIGNISHA BODY yao mmy dimpoz, hali kadhalika ben paul naye katoa video kali, izzo busnes, mwana fa , ni video kubwa sana

Saturday, December 19, 2015

arsenal yetu

Aesanal ni klabu iliyopo kaskazin mwa jiji kongwe nchini england miongoni mwa majiji ya nchini humo yaliyo na timu nyingi zinazo cheza ligi kuu, mfano westham united, qpr,tottenham spurs,chelsea na arsenal hizo baadhi tu zilizopo kule ila kuna timu kama kumi leo makala hii itahusu zaidi timu ya arsenal ambayo makao makuu yake yapo pale emirate studium kaskazin mwa london kuna maswali mengi yakujiuliza kuhusu timu hii
unaweza kujiuliza kwanini arsenal kwa miaka hii ya karibuni haija chukua vikombe hususani EPL maana kila mshabiki wa soka barani humo ukimuuliza atakwambia miaka 11 bila ya kombe ataanza kucheka na kumtupia  neno arsenal
kwanini arsenal haichukui komnbe? hili ni swali zuri sana la kujiuliza hali yakuwa mara nyingi timu hiyo inaaanza vizuri

jibu: arsenal haina lengo la baya kabisa bali  vitu viwili vinavyo isumbua arsenal 1.wenger  2. majeruhi wenger ina igharimu vipi arsenal kiburi chaake cha kutotaka kujua kuwa falsafa yake imefeli sasa ina bidi afanye mixing ili kusaidia wale waliopo hii ni sababu kubwa inayo msumbua mzee wenger,, kwa kikosi kilichopo si kibaya bali  ubaya mzee kutotaka kukubali kuwa inahitajika watu wa kuziba vilaka katika timu yake,, yaani quality player( wachezaji wenye ubora)  kama angekuwa mwepesi kukubali hilo aisinge pata taabu naamini angechukua vikombe
2.majeruhi arsenal  kila ifikapo mwezi wa 11 kila mwaka najeruhi hawakosekani kwa mfano dany welbeck,jack wilshare,Aaron ramsey,alexis sanchez,theo walcot oxide chamberlain,ospina,, koscienly, per metersacker,cazorla,rosicky debuch, coquelin,arteta na wengine walikuwa wanaumwa na bado wanaendelea kuumwa kipindi ambacho arsenal inawahitaji sana hii ili kuwa pigo kubwa naamini wachezaji wamekosa hali ya kujiamini baada ya wenzao kupata majeraha na hali ya kawaida  wachezji wanao pata nafasi ya kuanza mara kwa mara wakiumia kwa mkupuo timu inakuwa katika wakati mgumu sana na hili lina ikumba arsenal kila mwaka na sijajua madokta wao wnafanya nini na kwanini kila mwaka iwe kwa arsenal na si timu nyinge hili nalo swala la pili linalo isumbua arsenal
3. mzee wenger amefanya makosa makubwa sana katika kipindi hiki cha karibuni kama arsenal wasinge uza wachezaji wake  key player walio kuwepo kipindi hiko hivi sasa arsenal ingekuwa kama brcelona kuanzia 2008 haadi 2013 alivyo malizia kuuza van persie hebu angalia list hii, ROBIN VAN PERSIE,, SAMIR NASRI, GAEL CLICH,CESC FABRIGAS,ALEXANDER HLEB,EMANUEL ADEBAYOR,.ALEX SONG. hawa wote wasinge uzwa kwa vipindi hivyo na kubaki nae hivi sasa arsenal ingekuwa timu nyingine ukiangalia hao walikuwa katika link ya kidunia kabisa hili pia ni kosa kubwa

kwa kipindi hiki kilicho baki ubingwa uko wazi kwa yoyote yule kati ya wafuatao, arsenal,manchester united na manchester city hii ligi haitabiliki kabisa huyu leicster city  atahangaika mwisho wa siku atambania  mkubwa mmoja kuingia top four ila kwa maono yangu kuchukua ubingwa hapana,,

Thursday, December 17, 2015

vanesa mdee nae awa mtanznaia watano kufikisha followers milion moja

Baada ya  dimond platnumz kufikisha followers milion moja miezi miatu iliyo pita akafuatiwa na wema sepetu kufikisha idadi hiyo baada ya hapo akaja mtangazi maarufu wa amplifaya millard ayo baaada milardy ayo kijiti kikaja kwa  joketi mwongela akawa wanne sasa vannesa mdee nayo kafikisha followers milion moja


kwa kawaida ya wengi waliopita baada ya kufikisha idadi hiyo huwa wanaweka mbwembwe zao ila tofauti  na v0money yeye bado haja weka kitu hongera vanesa unastahili

Wednesday, December 16, 2015

elimu bure january dk john pombe magufuli

Akijibu swali la fedha zitapatikana wapi za kutimiza ahadi yake ya elimu ya bure, Magufuli amesema, mwezi huu wa Desemba pekee, Tanzania inatarajiwa kukusanya kiasi cha dola bilioni 1, ambazo hazijawahi kukusanywa.Amesema kuanzia mwezi huu fedha za kusomesha wanafunzi bure zitaanza kutengwa kuanzia mwezi huu.Kwa mujibu wa Dkt Magufuli, Serikali imefikia uamuzi wa kutenga dola milioni 65.5, ambazo zitapelekwa moja kwa moja katika shule zenye uhitaji na kwamba fedha zitakapotumwa, nakala ya barua itapelekwa kwa mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya pamoja na mkurugenzi wake.Rais Magufuli ameonya yeyote atakayetumia fedha hizo vinginevyo kwamba atachukuliwa hatua kali.Amesema fedha hizo zitasaidia katika ununuzi wa vitu kama vile chaki, maandalizi ya mitihani na vitu vingine vya muhimu shuleni.

zigo remix

Ay yupo south africa kwa ajili ya kushoot video yake ya ZIGO huku akionekana akiwa na dimond platnumz katika cover photo ambayo ilitolewa na kampuni anayo shoot nayo huku ay akifanya vitu vyake kimya kimya12345912_1111893075502144_366327264_n
mnamo mwezi wa watatu AY alifanya mahojiano na BONGO 5  na alisema kuwa kuna watu wengi hakuwza kuwataja ila amesema ni wengi mmoja wapo ndio tayari tusha mfahamu tunasubiri

Tuesday, December 15, 2015

christiani bella kuja na bella house of talent

christian bella obama anakuja na project yake ya kusaidia vipaji vya muziki, anakuja na bella house of talent ili kusaidia upande wa pili wa wasanii wachanga muimbaji huyo wa WACHA KABISA ambayo ameitoa hivi karibuni akimshirikisha koffii olomide amesema atasaidia vijana kwa staili hiyo


katika project hiyo amesema aatafundisha vocal christian bella ameingia katika headline mwezi huu baada kuachia nyimbo alio imba na ALIKIBA   sasa hivi anaenda kushoot video yake ya acha kabsa na kofii olomide

Monday, December 14, 2015

GIROUD ni mchezaji wa Tatu kufunga magoli 50 EPL KWA ARSENAL

olivier giroud awa mchezaji wa saba kuingia rekodi za arsenal baada ya kuifunga aston vila kafikisha goli 50 katika mechi 113 ana kuwa mchezaji wa tatu kufunga magoli hamsini akiwa na mechi 113 wakatyi yeye aakifanya hivyo wachezaji wengine waliofika rekodi hiyo  ni KING THIERY HENRY yeye kafunga goli 50 kwa mechi 83 tu,,,
2F56C0DB00000578-0-image-a-24_1450049738140

deni berkanmkp amefikisha mabao 50 kwa mechi 114 wakati nafasi ya pili kwa wagungaji wa arsenal kwa haraka inashikwa na IAN wRIGHT kwa mechi 87 wengine ni ROBERT PIRES mechi 137 huku ROBIN VAN PERSIE  alifunga goli 50 akiwa na mechi 142 wa mwisho katika listi hii ni THEO WALCOT yeye amefunga magoli kama hayo kwa mechi 208


arsenal yakutana na MSN 16 bora





uefa wame panga hatua ya mtoano kwa mara nyinge arsenal yakutana na kisiki 16 bora makundi kama uonavyo hapo



Godbless Lema ndiye mbunge aliechaguliwa arusha

godbless lema ndiye mbunge wa arusha baada ya kufanyika uchaguzi wa ubugne hapo jumapili na kuibuka kura elfu 68 dhidi 35 elfu ya mpinzani wake wa chama cha mapinduzi Philimon mollel act wamepata kura  353 hivyo mbunge huyo kutetea tena kiti chake



Lema ataungana na wabunge wenzake bungeni kwa ajili ya kusaidia wananchi wake watakacho mtuma uchaguzi huo ulisimmishwa na kusogezwa mbele kutokana na sheria zilizopo na hivyo lema kuchaguliwa tena

Saturday, December 12, 2015

Wamechemka kutuchora sehemu ya pili ya makala

Baada  ya  mataifa mengi jirani kutuangalia kwa jicho la husda na kutaka kuona jinsi gani mwaka huu wa uchaguzi tutawezaje kumwaga damu kama zilivyo nchi zao hii sasa inaonesha dhahiri wamechemka kwakuwa  kile walicho kitarajia hakikuweza kupatikana, wengi wao walikuwa wanaangalia jinsi gani Tanzania wanamwaga damu na ilikuwa wazi kwani hata raisi wa Rwanda PAUL KAGAME  yeye ameweka wazi kabisa kabla uchaguzi kufanyika kuwa tunataka kuona Tanznaia inayo hubiri amani tuone mwaka huu,,
Hayo maneno yalikuwa na uzito mkubwa sana kwa taifa letu ambalo kwa bahati nzuri hatuna uchafu wa kuvurugika kwa amani,, ni kweli tuna uhuru wa amani ila sio uhuru wa maisha lakini ni tofauti kabisa na nchi nyingine za afrika hawana uhuru wa amani wala uhuru wa masiha vyote wamekosa ukivichanganya hivyo jibu lake umasikini najua wazi kuwa kuna viongozi ambao wana roho za viongozi wa burundi au rwanda congo na nchi nyingine zenye mgogoro lakini inapo fika swala la amani bado tunarudi kuwa kitu kimoja na tuna songesha taifa letu katika mstari ulio nyooka , hii ina maana kuwa Tanzania bado itaabaki kuwa kisiwa cha amaani japo amani ya nadhani lia amabapo kila mwananchi wake anaitazama amani hiyo kama tunu au lulu pekee ya maendeleo
Kagame alivyoona presha ya uchaguzi na mwamko uliopo kwa wa tanzania kutaka mabadiliko ya kimaendeleo walijua kabisa endapo mmoja kati ya lowasa au magufuli atakae anguka vurugu itaanza na waanze kufurahi kuwa kitumbua kimeingia mchanga kumbe si hivyo wafikiriavyo
Tanzania pamoja na majanga yote ya kikatili yaliyopo ila bado kuna imani kubwa ya kumuogopa mtu anae itwa amani,, AMANI,, hii inatupandisha chati ya dunia kupenda kutembelea nchi yetu na kufanya utalii mbali mbali
hii inatukumbusha kuwa amani tulie nayo na mali adhimu walie tuachia walio tangulia mbele ya haki hii ina maanisha kuwa  sisi binadamu hatuwezi kufurahia maendeleo ya mwigne hadi nae aingie katika matatizo
             


RAMANI YA TANZANIA IKIWA KATIKA UBORA WAKE NA JINSI MUNGU ALIVYO IPENDELEA UZURI

hii kwa sasa kuna vitu vingi vimechagizwa navyo raisi magufuli anafanya vizri na kuamua kutengeneza Tanzania mpya na bado tuna muombea dua mungu amjalie ili asirudi nyuma katika juhudi zake za kulikomboa taifa wale walio taka tugombane sasa wanaiiga mfano kutoka kwa raisi huyo kwa yale mazuri anayo yafanya ya kutumbua majipu kama ilviyo slogani yake
katika hili nimwambie magufuli asikate tamaa
 kablaya uchaguzi niliandika wanatuchora sasa hii ndio mrejsho wake



Friday, December 11, 2015

roberto wa amalula amsfia magufuli

ROberto wa AMRULA ametua dar kwa ajili ya show , akiongea na millard ayo tv reborto ameongea vitu vingi sana vya kuihusu Tanzania na wasanii wake alipo ulizwa juu ya kuzungunzwa kwa magufuli roberto amemsifia raisi magufuli tena kwa mifano
Roberto

roberto ameyasema mengi kuhusu dk magufuki kubwa alilo sema kiongozi huyu ni mfano mzuri wa kuigwa kwa wa afrika wote na atapata kitu cha kuongea akifika zambia juu ya serikali yake na raisi wa nchi hiyo roberto pia amesema magufuli anaongoza kwa mifano ni nadra sana viongozi kama hao kutokea afrika nampa saluti raisi wenu  siku chache alizo kaa na mabadiliko tuna yaona hivyo ndivyo kiongozi anatakiwa
roberto ambae amekuja katika show amesema kuwa vanesa mdee amefanya nae collabo na nyimbo iko tayari  pia kuna collabo na shetta  baada ya show atapata nafasi ya kuzunguza na uongozi wa alikiba pia uongozi wa dimond katika  kufanya nao kazi, mkali huyu wa hit single ya amalula ameongeza kuwa nyimbo  za tanznaia zinapigwa sana zambia hususani dimond planumz alikiba ,, vanesa mdee na feza kessy

semenya apata mwezna

caster semenya apata jiko mwana riadha nguli wa afrika kusini custar semenya amepata jiko  baada ya kuonekana  wakfanya ndoa ya kimila mwanariadha huyo ambaye inasemekana anajinsia mbili ameonekana yuko katika sherehe za kimila kuonesha yuko tayari kupata mwenza
Embedded image permalink

moja ya picha zilizo enea mtandaoni na gazeti la sport24 limeeleza undani wa sherehe hiyo ingawaje semenya mara kwa mara amekuwa akikataa kuhusishwa na kupata mwenza na kuwahi kusema hizo ni habari tu za kidaku ambazo umeziskia katika magazeti
Embedded image permalink
moja ya picha zikimuonesha akiwa katika sherehe hiyo

sorce SPORT24

Tuesday, December 8, 2015

ozil atajwa mchezaji bora wa mwezi november akiwa ju ya jamei vardy nachriss smalling

Kiungo wa arsenal ametajwa mchezaji bora wa mwezi november ligi kuu ya uingereza(pfa fans
Ozil alikuwa anashindana na beki wa Manchester United  Chris Smalling na Leicester striker Jamie Vardy.
Ozil pia ame kuwa mchezjai wa kwanza msimu huu ktk ligi tano kubwa kuwa ame saidia upatikanaji wa magoli zaidi, 
Ozil has 12 Premier League assists to his name this season
Ozil ame fanya usaidizi katika timu ya arsenal 12 msimu huu na kavunja record ya kusaidia mara sita mfululizo

koffi olomide amesema kama itatokea ana matumaini kufanya collabo na Dimond platnumz

msanii mkongwe barani afrika na duniani koffii Charles Antonio olomide amesa ana matumaini kabisa kama itatokea collabo na msanii wa bongo flava nchini nasib abdul ama dimond paltnumz akizungunza na millard ayo tv alipotua dar es salaam 07.12.2015 ameseama kuwa kama itakuwepo ana matumaini kufanya nae

 koffi alomide amabaye alikuwa tangu zamani na nyimbo yake iitwayo shamukwale,,, kwa sasa ana kibao kipya kinacho ichwa EKOTITE  ambaypo kimeoneka kuwa bamba vilivyo watanzania wengi
hizi ni baadhi ya nyimbo zake





Monday, December 7, 2015

belle 9 namuoa mbali

namuona belle 9 ehemu nyingine katika muziki wake,wakati wa Tanzania wengi waki pambana matui chuki na kudharauliana kati ya mashabiki wa alikiba for real na dimond platnumz kuna msanii mwingine ambaye mwaka 2016 huo utakuwa wake na atakuwa msanii mkubwa barani afrika na duniani kote, kwanini nimegusia na kuthubutu ukubwa wa belle 9
belle9 ni mzaliwa wa morogoro na amefanya nyimbo kali zote alizo wahi kufanya kifupi hazija wahi kubuma tangu atoe nyimbo zake na hilo halina ubishi kwa wasikiliza music swafi belle9 amefanya makubwa

moja ya watu ambao hana malumbano na mtu na anafanya muziki wake kwa utaratibu unao takiwa na pia anasubra,, bele 9 alishawahi kusema kuwa anacho mzidi dimond ni connection tu ila katika kuimba niko vizuri kuzidi yeye ,, hapa michukiulie bifu belle 9 ni muimbaji hodari sana na anavyo kuja sasa naona anakuja kivingine mara baada ya kutoa nyimbo yake  video
hivi sasa trace wanapiga nyimbo yake na pia kuna nyimbo nyinge inaitwa burger movie selfie,trace wamesema itakuwa


joketi mwongela awa mtanznia wa nne kufikisha followers milioni katika ukurasa wa instagram

joketi mwengelo  awa mtanzania wa nne kupata followers milion 1 wa kwanza alikuwa dimond akafuata wema sepetu  akaja millard ayo na sasa JOKET nae kafikisha followers milion moja



katika ukurasa  wake wa fecebook ame washukuru followers wake kwa kumfikisha hapo ameandika

GOOD MORNIGN , KISSES TO ALL  MY ONE MILLIONS ON INSTAGRAM,,, MU BUTHU BUTHU TELE KWENU NYOTE kwa kufikia milioni moja katika page yangu

Sunday, December 6, 2015

msimamo huu hapa baada ya mechi za weekend hii 05 12.2015 kabala ya mechi ya liverpool

alikiba profile yake kwa ufupi

wenye sauti laini kama siagi, Bwana Alikiba ni mfalme wa Tanzania kwa kila namna. Baada ya pumziko refu kwenye game ya muziki, alikiba arejea tena na ngoma kali balaa, zikiwemo: Mwana na Chekecha Cheketua. Alikiba ni sababu tosha kuamini kuwa vipaji Afrika vitadumu milele. Ni mfano bora wa jinsi gani wasanii wanaweza kududna na kurejea katika game. Usimkose mwandishi huyu katika Coke Studio Africa msimu wa 3.
SAFARI YAKE YA MUZIKI
Alikiba Saleh Kiba ni msanii, mwandishi wa mashairi, mtayarishaji, mchezaji, muigizaji na model kutokea Tanzania. Ni msanii wa Bongo Fleva, aina ya muziki unaotamba sana na kuimbwa na wengi Tanzania. Kutoka na kampuni ya utafiti ya Kenya, mwaka 2011, Alikiba alitajwa kama msanii alieuza nakala nyingi kwa Afrika Mashariki. 2009, Alikiba alitajwa katika tuzo za Africa Music Awards kama Best East African Artist kule Uingereza
WANAOMHAMASISHA KIMUZIKI
Alikiba is anahamasishwa sana na Usher.
BACKGROUND
Baada ya kumaliza shule mwaka 2004, Alikiba aliandika nyimbo yake ya kwanza “Maria” kisha akaendelea kutoa single baada ya hapo, zikiwemo; “Najuwa”, “Ndugu wangu”, “Kuteseka”, “Namshukuru Mungu”, “Sabrina”, “Yatima” na nyingine nyingi.
MENGINE KUHUSU
Alikiba anapenda mpira na kama asingefanikiwa kuwateka watu katika majukwaa ya muziki basi hakika angekuwa akiwakusanya watu katika viwanja vya mpira. Raisi wa Tanzania, Jakaya Kikwete alimtunuku Alikiba kwa ajili ya mchango wake mkubwa kwenye sanaa na tamaduni ya muziki Tanzania.
copy and pest from coca-cola website

Saturday, December 5, 2015

dawasco yapandisha bei ya maji

Dawasco yapandisha bei ya maji
Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco), limeanza rasmi kutumia bei mpya za ankara za maji, ikiwa ni siku chache baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (Ewura) kupitisha mapendekezo ya kupandisha bei kama walivyoomba.
Awali, Dawasco iliomba kuongeza bei ya utoaji wa huduma hiyo ili kuboresha huduma zake katika Jiji la Dar es Salaam, Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.
source as you see link above mwananchi communication .co.tz