karibu

kwa habari moto moto

Tuesday, December 6, 2011

IMANI ZA KISHIRIKINA MKOANI MTWARA

Wananchi wa mkoa wa mtwara wame choma moto pikipiki ya askari kwa hasira mara baada ya askari hao kusimamisha shughuli za utoaji uchawi,hayo yametokea baada ya waganga kufika kwenye eneo la mwenyekiti wa ccm ambapo mwenyekiti huyo mara alivyoona waganga hao wakifika eneo lake akaamua kuwapigia simu polisi kwa madai ya kufanyiwa fujo eneo lake hivyo askari hao walikuja kusimamisha tukio hilo
ndipo wananchi wenye hasira kali kuamua kuwashambulia askari hao na kuunguza pipiki hiyo askari wanaripoyiwa kuwa hospitali kwa matibabu

ARSENA YA PIGWA 3-1

WAKATI MZEE ARSENAL VENGER KUWEKA WATOTO KATIKA TIMU YA ARSENAL HAPO JANA TIMU HIYO IMETANDIKWA GOLI 3 KWA MOJA GOLI LA ARSEANAL LIMEFUNGWA NA MWISLAEL YOSSI BENAYOUN KWA SHUTI KALI HILI NI GOLI LAKE LA KWANZA LIGI YA MABINGWA TANGU ATUA GUNNERS
LUKAS FABIANSK ALIUMIA NAFASI YAKE ILICHUKULIWA NA MONOINE AMBAYE ALIDAKA MADUDU NA KUTANDIKWA GOLI MBILI ZA HARAKA HATA HIVYO ARSENAL IMEFUZU HATUA YA 16 BORA  KWA KUSHIKA NAFASI YA KWANZA IKIWA NA POINT 10 KIBINDONI

HAYO YAKIENDELEA WATOTO WA AVB WAMEONA MWEZI BAADA YA DIDIER DROGBA KUFANYA KAZI YA ZIADA NA KUIPATIA MABAO MAWILI HUKU MBRAZILI RAMIRES AKIKAMILISHA MAGOLI 3 YA CHALSEA.PASI YA MATA ILIMFANYA DROGBA KUPATA  BAO LA KWANZA KISHA DROGBA KUSABANISHA PASI YA GOLI LA RAMIRES BAADAE MATA AMETOA PASI ADIMU AMBAPO DROGBA HAKUFANYA AJUZA NA KUUKWAMISHA KIMIANI
MATOKEO MENGINE AC MILAN WAMETOKA SULUHU YA MABAO 2 KWA 2 NA PLZEN HUKU BARCA WAKIIKANDAMIZA BATE BAO 4 KWA UBUYU

Friday, October 28, 2011

TAKUKULU MKOANI MTWARA WAANZA KUSAKA WATOA NA WAPOKEAJI RUSHWA

MKUU WA TAASISI YA KUZUIYA NA KUPAMBANA NA RUSHWA MKOANI<TAKUKULU> MTWARA BWANA AIDANI NDOMBA AMEWAOMBA WANANCHI WA MKOA WA MTWARA KUSHIRIKIANA KATIKA KUWATAJA WAPOKEA NA WATOAJI WA RUSHWA  ILI WAFIKISHWE KATIKA VYOMBO HUSIKA VYA SHERIA

HAYO AMEYASEMA AKIWA OFISINI KWAKE NAKUSEMA WANANCHI WA MTWARA WAPO NYUMA KATIKA KUTOA TAARIFA ZA WAHARIFU HIVYO KURUDISHA NYUMA MAENDELEO

AIDHA BWANA NDOMBA AMESEMA  ELIMU INATOLEWA SEHEMU MBALIMBALI ILI KUWEZA KUWAELIMISHA WATU WAACHE UOGA WA KUWATAJA WAHALIFU

Thursday, October 20, 2011

SHIRIKA LA NYUMBA MKOA MTWARA LIMEGUNDUA NJIA MPYA YA KUWADHIBITI WATEJA WANAOWADHULUM HAKI ZAO

SHIRIKA LA NYUMBA  LA TAIFA <NHC>MKOANI MTWARA LIMEAMUA KUWEKA NJIA RAHISI ILI WAWEZE KUFUATILIA NYUMBA ZAO KWANI WAPANGAJI WA NYUMBA HIZO WANA WAPANGISHA WAPANGAJI WENGINE NA KUFUJA KIPATO CHA NYUMBA HIZO

WAKIZUNGUMNZA KWA NYAKATI TOFAUTI WAMILIKI HALISI WANYUMBA HIZO WAMESEMA KUNA NYUMBA TANO AMBAZO  ZILIKUWA  ZINATUMIKA BILA YA  MPANGILIO  NA KUTOLIPA  NYUMBA HIZO PIA KUNA UBADHILIFU WA ZAIDI YA LAKI 200,000 AMBAZO WAPANGAJI WAMEPANGISHA NA KUJIONA HAO NDIO WENYE NYUMBA HIZO

AIDHA WAMILIKI HAO HALALI WAMESEMA KUWA HIVI SASA WANA WAPANGISHA KWA MKATABA WA MWEZI MMOJA MMOJA ILIKUONDOA TATIZO  HILO KUBWA MKOANI MTWARA

Tuesday, October 11, 2011

WAHADHIRI WA CHUO CHA SAUTI WAIZUNGUMZIA MIAKA 50 YA UHURU KWA NAMNA YAKE

Wahadhiri wa chuo kikuu cha sauti mkoani mtwara waizungumnzia miaka 50 ya uhuru kwa namna yake ambayo tuna adhimisha tarehe 9 december mwaka huu hayo yalisemwa jana na doctor AIDANI MSAFIRI wakati aklizungumnza na waandishi wa habari ofisini kwake

Doctor msafiri amesema tenasherehekea miaka 50 ya uhuru lakini amani haipo serikali asidhani kuwa kupigana ndio uvunjifu wa amani,amani ni ile hali ya kupata kile unacho kihitaji endapo hauna chakula hiyo siyo amani iliyo kusudiwa pia amehoji shule,barabara hospitali zipo lakini zina uboro kwa maana wafanya kazi wenye elimuwapo, zte hizo ni cha ngamoto ambazo serikali inabidi ijipange

pia amehoji ndani ya siasa kunavitu vitatu muhim vipo 1.uwazi-transparent 2.uwajibikaji-responsibility 3.maadili-ethics mambo hayo ndani ya democrasia ya tanzania hakuna ndani ya miaka 50 pia ameomba serikali iwajibike pamoja na wananchi ili tupeleke mbele taifa letu

Naye mhadhiri afisa tawala na mipango chuoni hapo ndugu GAMA yeye amesema mabadiliko yapo mengi sana kulinganisha na zama zile za uhuru ametolea mfgano zamani kutoka mtwara kwenda da re ssalaam walitumia siku tatu sasa masaa 8 upo dar er salaam pia kuna hospitali na shule kila kata naye ameiomba serikali iwajibike na asimame kama serikali ili waimarike zaidi katika utendaji wa kazi kwan isasa serikali ina changamoto ya ukosefu wa umeme

Monday, October 10, 2011

WAFANYA BIASHARA SOKO KUU MTWARA WALALAMIKIA UONGOZI

WAFANYA BIASHARA WA SOKO KUU MTWARA WAILALAMIKIA  UONGOZI WA SOKO HILO KWA KUTOWAJIBIKA IPASAVYO HAYO YALISEMWA NA WAFANYA BIASHARA WA SOKO HILO WALIPO DAI USAFI WA SOKO HILO HAULIDHISHI  PAMOJA NA MIPANGO MIBOVU YA VIONGOZI HAO

AIDHA MFANYABIASHARA JUMA NYENJE YEYE AMETOA LAWAMA ZAKE UFUNGUAJI  WA CHOO WANACHELEWA HIVYOKUSABABISHA WATU KUJISAIDIA KWENYE CHUPA HIVYO ANAWAOMBA VIONGOZI WATILIE MKAZO SWALA HILO ILI YASITOKEE MAGONJWA YA MLIPUKO

AIDHA MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAFANYABIASHARA WA SOKO HILO BWANA NYAMBI LUYEYE KWA UPANDE WAKE AMEKANUSHA NA KUSEMA SHUGHULI ZOTE ZINAENDA SAWA USAFI UNAENDA SAWA WAPO WANAO SAFISHA ILI AMEWAOMBA WAFANYA BIASHARA HAO USAFI UNAANZIA KWAO WENYE WAWEKE SEHEMU MOJA UCHAFU PINDI WAFANYA USAFI WATAKAPO PITA WAUKUTE UPO SEHEMU MOJA

Saturday, October 8, 2011

KUSHUKA KIWANGO CHA ELIMU SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI MKOANI MTWARA

IMEELEZWA KUWA UTORO, MAHUDHURIO HAFIFU,TATIZO LA MIMBA SHULENI, UPUNGUFU WA MIUNDOMBINU ILIYO BORA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI NICHANGAMOTO ZINAZOIKUMBA ELIMU MKOANI MTWARA

HAYO YAMEBAINIKA LEO KATIKA MDAHALO WA ELIMU  ULIOFANYIKA KATIKA CHUO CHA UALIM MASANDUBE MTWARA
MDAHALO HUO ULIOANDALIWA NA MTANDAO WA KIRAIA WA MARENGO UMEHUDHURIWA NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MTWARA MIKINDANI BI MAGRETH  NAKAINGIA WENYEVITI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MTWARA MIKINDANI WANAFUNZI,WADAU WA RADIO  NA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM

AIDHA TAARIFA YA AFISA ELIMU MKOA WA MTWARA BW KIPANYA AMEELEZA KUHUSU HALI YA MAENDELEO YA ELIMU MKOANI MTWARA  KUANZIA MWAKA 2005 HADI 2010 INASEMA KUWA MKOA WA MTWARA ULIKUWA NA JUMLA YA SHULE 563 ZA MSINGI ZILIZOKUWA NA WANAFUNZI 224,890. AMBAPO SHULE 561 ZILIKUWA ZA SERIKALI NA SHUKE2 ZILIKUWA ZA WATU BINAFSI LAKINI MWAKA HUU 2011 SHULE ZA MSINGI 626  AMBAPO ZA SERIKALI NI 622 NA BINAFSI 4 AMBAZO ZINAJUMLA YA WANAFUNZI 244,240

PAMOJA NA KUWEPO KWA ONGEZEKO LA SHULE 63 ZA MSINGI HALI YA UFAULU IMEENDELEA KUDOLOLA MWAKA HADI MWAKA KUTOKA 68.3%  MWAKA 2006 HADI 47.7% MWAKA 2010

KWA UPANDE WA ELIMU YA SEKONDARI MKOA ULIKUWA NA SHULE 53 MWAKA 2005 ZENYE JUMLA YA WANAFUNZI 11,381 HADI SASA KUNA SHULE ZA  SEKONDARI 137 ONGEZEKO LA SHULE 73 ZILIZO JENGWA KWA USHIRIKIANO WA SERIKALI NA NGUVU ZA WANANCHI NA TAASISI BINAFSI

Friday, October 7, 2011

PUSHA-T ATANGAZA TAREHE YA KUINGIZA SOKONI ALBAM YAKE YA `fear of GOD 2

RAPA PUSHA-T AMETANGAZA TAREHE RASMI YA KUINGIZA SOKONI ALBUMU YAKE MPYA INAYOJULIKANA KAMA ;fear of God 2 , let us pray,AMBAYO ITAINGIA SOKONI KWA KUSHIRIKIANA NA LEBEL YA KANYE WEST YA G.O.O.D MUSIC IMPRINT 

ALBUM HIYO ITAKUA NA NYIMBO 12 SAMBAMBA NA XCLUSIVE VIDEO NNE ITAKUA SOKONI NOVEMBA 4,2011 NA KATIKA ALBUM HIYO   KUNA COLLABO ZA KUTOSHA

KAMA VILE  RICK ROSS,DIDDY,KANYE WEST, TYLER THE CREATOR NA WENGINE WENGI

FEAR OF GOOD 2   CHECK NGOMA ZILIZOMO
1.CHANGING OF GUARD FT DIDDY
2.RAID FT 50 CENT
3.SO OBVIOUS
4.TROUBLE ON MY MIND FT TYLER,THE CREATOR 
5.ISTILL WANA FT RICKROSS
6.ALONE IN VEGAS
NANYINGINE NYINGI TU SUBIRI HADI MDA HUO  WA NOVEMBA UPATE VITU KUTOKA KWA MTU MZIMA PUSHA-T

Thursday, October 6, 2011

MAENDELEO YA MITIHANI YA TAIFA MKOANI MTWARA KIDATO CHA NNE

WANAFUNZI WANAO HITIMU ELIMU YA SEKONDARI KATIKA SHULE YA SEKONDARI SABASABA  KUTWA MKONI MTWARA WANA MATUMAINI MAKUBWA  YA KUFAURU  MITIHANI HIYO INAYOENDELEA MCHINI TANZANIA 

AIDHA WALIMU WA SHULE HIYO WALIPO ZUNGUMNZA NA WAANDISHI WA HABARI WAMESEMA MATUMAINI YAPO INGAWAJE SIMAKUBWA KUTOKANA NA MAANDALIZI KUWA DUNI NA MATOKEO MABAYA YA MTIHANI WA MOCK  ULIOFANYIKA AUGUST MWAKA HUU

NAYE  MKUU WA SHULE HIYO MR SANGA  AMESEMA UVIVU  WAWANAFUNZI HAO WA KUJISOMEA PAMOJA NA WAZAZI WAO  KUTOJUA UMUHIMU WAELIMU NDIO SABABU KUBWA YA KUSHUKA KWA KIWANGO CHA ELIMU SHULENI HAPO, PIA AMEWAOMBA WADAU , WAZAZI NA WAANDISHI WA HABARI KUSHIRIKIANA NA SHULE HIYO KATIKA KUWAHIMIZA WANA FUNZI ILIWAWEZE KUELEWA MAANA HALISI YA ELIMU

Wednesday, October 5, 2011

MADAI YA KURUDIWA KWA UCHAGUZI MTWARA MJINI

Baada ya kufungua kesi ya kubatilisha uchaguzi wa ubunge uliofanyika  30.10. 2010  kutokana na masharti ya uchaguzi huo kuvunjwa na msimamizi wa  kuhesabu kura kutenga ukumbi mwingine wa T.C.C  kuhesabu kura hizo  badala ya ukumbi uliopangwa wa  manispaa ,
Hayo ni maelezo ya mfungua kesi hiyo ndugu  ULEDI HASSANI ABDALLAH aliye gombea ubunge kupitia chama cha C.U.F wakati akitoa maelezo kwa jaji bwana SULEIMANI SAIDI KIHIYO kuomba mahakama hiyo ibatilishe ushindi wa HASNIN MOHAMEDI MURIJI mgombea wa ccm kutokana na
kutotendewa haki wakati wa kuhesabu na kutangaza matokeo
Aidha katika majumuisho hayo pia wakili wa upande wa mdaiwa  JOSEPH KADAYO na FARAJI MCHIMBI  wao wamepinga maelezo hayo hayana ushahidi wa kutosha  kutokana na ushahidi huo kutolewa kwa mdomo bila ya nyaraka yeyote
Aidha baada ya kuhitimisha majumuisho hayo jaji wa kesi hiyo  bwana SULEIMANI SAIDI KIHIYO ameahirisha kesi hiyo hadi octoba 18 hukumu itakapo tolewa