karibu

kwa habari moto moto

Wednesday, October 5, 2011

MADAI YA KURUDIWA KWA UCHAGUZI MTWARA MJINI

Baada ya kufungua kesi ya kubatilisha uchaguzi wa ubunge uliofanyika  30.10. 2010  kutokana na masharti ya uchaguzi huo kuvunjwa na msimamizi wa  kuhesabu kura kutenga ukumbi mwingine wa T.C.C  kuhesabu kura hizo  badala ya ukumbi uliopangwa wa  manispaa ,
Hayo ni maelezo ya mfungua kesi hiyo ndugu  ULEDI HASSANI ABDALLAH aliye gombea ubunge kupitia chama cha C.U.F wakati akitoa maelezo kwa jaji bwana SULEIMANI SAIDI KIHIYO kuomba mahakama hiyo ibatilishe ushindi wa HASNIN MOHAMEDI MURIJI mgombea wa ccm kutokana na
kutotendewa haki wakati wa kuhesabu na kutangaza matokeo
Aidha katika majumuisho hayo pia wakili wa upande wa mdaiwa  JOSEPH KADAYO na FARAJI MCHIMBI  wao wamepinga maelezo hayo hayana ushahidi wa kutosha  kutokana na ushahidi huo kutolewa kwa mdomo bila ya nyaraka yeyote
Aidha baada ya kuhitimisha majumuisho hayo jaji wa kesi hiyo  bwana SULEIMANI SAIDI KIHIYO ameahirisha kesi hiyo hadi octoba 18 hukumu itakapo tolewa

No comments:

Post a Comment