karibu

kwa habari moto moto

Saturday, October 8, 2011

KUSHUKA KIWANGO CHA ELIMU SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI MKOANI MTWARA

IMEELEZWA KUWA UTORO, MAHUDHURIO HAFIFU,TATIZO LA MIMBA SHULENI, UPUNGUFU WA MIUNDOMBINU ILIYO BORA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI NICHANGAMOTO ZINAZOIKUMBA ELIMU MKOANI MTWARA

HAYO YAMEBAINIKA LEO KATIKA MDAHALO WA ELIMU  ULIOFANYIKA KATIKA CHUO CHA UALIM MASANDUBE MTWARA
MDAHALO HUO ULIOANDALIWA NA MTANDAO WA KIRAIA WA MARENGO UMEHUDHURIWA NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MTWARA MIKINDANI BI MAGRETH  NAKAINGIA WENYEVITI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MTWARA MIKINDANI WANAFUNZI,WADAU WA RADIO  NA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM

AIDHA TAARIFA YA AFISA ELIMU MKOA WA MTWARA BW KIPANYA AMEELEZA KUHUSU HALI YA MAENDELEO YA ELIMU MKOANI MTWARA  KUANZIA MWAKA 2005 HADI 2010 INASEMA KUWA MKOA WA MTWARA ULIKUWA NA JUMLA YA SHULE 563 ZA MSINGI ZILIZOKUWA NA WANAFUNZI 224,890. AMBAPO SHULE 561 ZILIKUWA ZA SERIKALI NA SHUKE2 ZILIKUWA ZA WATU BINAFSI LAKINI MWAKA HUU 2011 SHULE ZA MSINGI 626  AMBAPO ZA SERIKALI NI 622 NA BINAFSI 4 AMBAZO ZINAJUMLA YA WANAFUNZI 244,240

PAMOJA NA KUWEPO KWA ONGEZEKO LA SHULE 63 ZA MSINGI HALI YA UFAULU IMEENDELEA KUDOLOLA MWAKA HADI MWAKA KUTOKA 68.3%  MWAKA 2006 HADI 47.7% MWAKA 2010

KWA UPANDE WA ELIMU YA SEKONDARI MKOA ULIKUWA NA SHULE 53 MWAKA 2005 ZENYE JUMLA YA WANAFUNZI 11,381 HADI SASA KUNA SHULE ZA  SEKONDARI 137 ONGEZEKO LA SHULE 73 ZILIZO JENGWA KWA USHIRIKIANO WA SERIKALI NA NGUVU ZA WANANCHI NA TAASISI BINAFSI

No comments:

Post a Comment