karibu

kwa habari moto moto

Friday, March 18, 2016

mbowe na uteuzi wake

Mwenyekiti wa chadema mheshimiwa Freeman Mbowe kafanya yale aliyo yafanya Dk John pombe magufuli katika uteuzi wake wa katibu mkuu.

kwanini na thubutu kusema hayo labda turudi nyuma  baada ya kuchaguliwa kuiongoza nchii hii kwa awamu ya tano dk John pombe magufuli kitu ambacho watu walitegemea kuteua waziri mkuu ambae wote walijua Mh Herison mwakyembe  hili halina ubishi ndani yake

kila mtu alikuwa na matumaini makubwa kuwa mwakyembe kutokana na kasi yake  wangeendana na magufuli 

kwa mshangao na hali isiyo tarajiwa magufuli amemteua mh Kassim Majaliwa kuwa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,  sio kwamba majaliwa hakuwa ana fahamika la hasha majaliwa alikuwa anafahamika ila wengi hawakudhani atakuwa waziri mkuu hata kwa 1% kasi yake na utawala wake baada ya kupewa nafasi hiyo watu tunaiona sasa

turejee katika mada kuu usiku wa kuamkia jumapili baraza kuu la chadema lilikuwa na kikao kizito ambacho ilikuwa ina mtafuta mtu ambae ata vaa viatu vya dk wilbroad slaa ambae aliachia ngazi kipindi cha uchaguzi mkuu 2015 baada ya kutofautiana na washirika wenzake mara baada ya kumkaribisha Edward lowasa na kumsimamisha kuwa mgombea wa chadema na ukawa 

Mbowe naye ikampata ya magufuli alikuwa na changa moto hiyo ya kumchagua katibu mkuu naaminimajina yalikuwa mengi na labda watu walikuwa na hisia tofauti na huyu akie chaguliwa, nilipata kusikia watu wengine wakisema mh LISSU wengine Salim mwalim lakini yote kapuni

bila ya uoga mh vicent masinji amechaguliwa kuwa katibu mkuu wa chama hiko ambae nae hakuwa anatajwa na wengi na watu hawakutarajia kama masinji atakuwa katibu mkuu

hii ina msaidia mbowe kutopata maswali mengi  kutoka kwa waandishi mbali mbali kutokana na  ushujaa huu wa kuchagua mtu asiye fahamika baadae anafanya kazi ambayo wengi inakuwa kama mshangao kama ilivyo kwa majaliwa

hii sasa inakomesha dhana ya mapendekezo ya watu pasipo ufuatiliaji kuwa nani anafaa na anaweza endesha sisa katika mlengo wa maendeleo

binafsi mimi mtoa makala simfaham sana lakini hii ya kutushtukiza ina leta tija kuliko hii tulie zoea. sijajua kama ndio sisa inakua au vipi jibu unalo wewe .

kikubwa na heri tuombe amani ya nchi yetu ili isiingie machafuko tuweze kuona mengi ambayo hatukuweza kuyaona katika vipindi vilivyo pita.

oprah ilinipa umarufu -irine uwoya

Msanii wa filamu za Tanzania Bongo movie IRENE UWOYA ameweka wazi wakati anaanza sanaa wazazi wake hawakuwa kutaka afanye kazi hiyo.

Uwoya filamu yake ya awali ilikuwa inaitwa 'DIVISION OF LOVE' kabla ya kufanya OPRAH ambayo imempa umaarufu mkubwa katika filamu hiyo ambayo wapinzani wakubwa kipindi hiko Ray kigos na Steven kanumba walikuwepo katika filam hiyo.ameyasema hayo e.fm kipindi cha uhondo.

Uwoya ambae ana mtoto mmoja aitwaye Crishna amesema filamu hiyo ilimfanya apate mafanikio na hata mme wake ambae amezaa mtoto Suleimani Ndikumana alimueleza kuwa hiyo movie ndio sababu ya kumpenda hadi kumuoa.

amewaasa wasanii wachanga haswa wakike kuwa wabunifu hata wakiwa katika tasnia hii wajaribu kuwa wabunifu ili wapate nafanikio zaidi. 

kuhusu uhusiano na msami amesema  kwa sasa yupo "single" hana mtu na kuhusu ndikumana ameomgeza kuwa hawajaachana kwani hakuna talaka iliyotoka ila kwa sasa wako mbali

uwoya atakuwa na movie yake inayoitwa kisoda na pia mambo mengine mazuri yanakuja

wenger na mustakabli wake

Arsene Wenger ana nafasi ya kuamua  kuwa timu yake iweje ili kama bado anahitaji kubaki emirate na kuwafanya mashabiki zake kupata amani kama ilivyo kwa timu nyingine

nathubutu kusema hayo kwakukiona kikosi cha arsenal na nikilinganisha kipindi barcelona wana pita katika kipindi kama hiki, mwaka 1999 hadi 2003 barcelona hakuweza kuchukua kikombe chochote miaka hiyo walikuwa wana pigania timu yao iweje 
japo nyakati zinatofautiana maana arsenal asipo pata taji lolote msimu huu itakuwa msimu wake wa 12 bila ya kuchukua kombe kubwa

arsenal sio mbaya lakini kuna vitu vingi vinakosekana pale wachambuzi wengi waliitabiria mafanikio makubwa arsenal msimu huu lakini haikuwa hivyo maana sasa kombe lililo baki ni epl ambalo amepitwa alama 12 na kinara wa ligi hiyo Leicester city. 
wenger anaweza kuamua kuwa atumie pesa zilizopo ili arudishe heshima iliyokuwa zamani ukilinganisha kikosi kile ambacho hakikufungwa msimu wa 2003-2004 ''unbeaten'' na ukilinganisha na hiki kilicho pambana na barcelona utaona utofauti 
kikosi hiki hakina watu kabisa una mtanguliza olivier Giroud ambae thiery henry alisha sema wenger huwezi chukua ubingwa ukiwa na Giroud. Hii inaonekana dhahiri kabisa ukosefu wa mmaliziaji ndio tatizo la arsenal msimu huu 
barcelona japo wana watu watatu wakubwa ambao wanaweza kuleta matokeo muda wowote lakini pia wana fungika, Danny welbeck amekosa nafasi mbili za wazi na theo walcot amekosa moja ya wazi ambapo kama zile nafasi angeipata aguero,cavan,lewandowsk au diego costa tungeona matokeo yana badilika pengije hata arsenal ingeweza kupita hatua inayofuata lakini ukosefu wa utulivu na thamani ya washambuliaji wa arsenal inawakosesha nafasi ambayo ilikuwa adimu kwa miaka mitano.
WENGER AFANYEJE?
wenger kama ana hitaji kubaki na kuendelea kutesa ina muhitaji achukue fungu la pesa kisha asafishe sehemu ya mbele yote ya arsenal, olivier giroud ,theo walcot, ,arteta,flamini chamberlen,rosicky na per metersacker wote inatakiwa watumbuliwe majipu. na na achukue watu ambao wataweza kumletea heshima ambayo kaipoteza kwa miaka 12.
achukue nani nani hapo sasa nadhani kila mtu anaweza kuchangia kuwa viwango vya kidunia mfano wa lewandowsk,isco, na aubamayang huo mfano tu ambapo wataweza kubadili arsenal kutoka kudhalauliwa hadi kuheshimika kuna vitu vingi vimekosekana arsenal haswa ushambuliaji.

NINI KINA ITAFUNA ARSENAL
kikubwa kinacho itafuna arsenal morali na kiongozi mkali anaye weza kuongea na wachezaji kwa ukali pia kwa upole kwa hamasa walie iamsha na barcelona hatua ya pili ile ndio wanatakiwa waende nayo hadi ligi kuu sasa hakuna wakuweza kuwa fokea pindi  wanapo zembea pia kocha dhaifu Ferguson mara nyingi kama mlicheza vibaya ndani ya uwanja mtakuja kukiona katika vyumba vya kubadilishia nguo hii wenger hana kabisa ambayo pia ni muhimu kwa kiongozi. 

USHAURI
pia kama hataki kubadili falsafa yake njia rahisi anaweza kuondoka tu ili atoe nafasi kwa wengine lakini bado simtoi miongoni mwa makocha bora barani  ulaya 

lugha chafu hazitakiwai katika michezo

Mkuu wa kitengo cha habari wa timu ya simba Haji Manara amewataka wa Tanzania kuacha kejeli za kudharau kaya au kabila fulani wakati wa kutoa matamshi yao.

hayo ameyasema wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha michezo cha asubuhi cha e.fm kinachoendeshwa na omary Katanga.

hayo yamekuja mara baada ya muda Jeri Muro kulisema kabila la Kizaramo ambali ndio kabila lake Haji Manara ambae ametanabaisha kuwa kabila hilo ndilo lililo anzisha yanga na simba, Yanga1935 na 1936 kwa Simba.

ushabiki na utani wa jadi utabakia pale pale wala hauwezi kuisha ila sio kutoa thamani ya utu hali ya kuwa jioni wanakaa wote kaitka vijiwe vya kahawa.

pia Haji hakubaliani na Tff kuwa achia viporo vingi yanga na azam ambao walikuwa katika michezo ya kimataifa. hadi sasa yanga ana viporo 2 azam 2 .

kabla ya kumaliza mahojiano hayo manara amewaomba waandishi wa habari atakuwa na taarifa kwa vyombo vya habari .